Jeshi la polisi Mkoani Mbeya
limelazimika kufanya kazi ya ziada kumuokoa mwanamke aliyefahamika kwa
jina la Hawa Mwalongo (30), mkazi wa Mtaa wa Mwambenja, Kata ya Iganzo,
Jijini Mbeya.
Tukio hilo limetokea Mei 4 mwaka huu
majira ya Alfajiri mtuhumiwa akiwa na mwanae Alfonce Mwalongo (miezi
mitano), alikutwa akiwa uchi huku mwanae huyo akiwa mita chache kutoka
kwenye nyumba aliyopanga inayomilikiwa na Bwana Mashaka Seke.
Mmoja kati ya mashuhuda ambaye ni
jirani yake amesema walisikia mtoto akilia alfajiri ndipo waliamua
kutoka nje na kumkuta Bi Hawa akiwa mtupu na walipomsemesha, alisema
anatoka Bunju Dar es salaamna kwamba anelekea Mbeya na walipomuambia
nguo zipo wapi hakuwa tayari kueleza na kutoelewa kinachoendelea.
Ameongeza kuwa amesafiri na lori
lililokuwa na Container na kufika hapo baada ya kufukuzwa na baba yake
mlezi aitwaye Esco Sikazwe, baada ya kutelekezwa na mumewe Bwana Nikas
Mwalongo.
Uchunguzi umebaini kuwa mwanamke huyo
alitelekezwa na mumewe kutokana na ujauzito wa mwanawe Alfonce, kisha
kuhamia kwa baba yake mlezi ambaye alimfukuza kutoka Mtaa wa Mwakibete
jijini hapa hali iliyomlazimu kwenda kupanga eneo la Ilemi majuma mawili
yaliyopita.
0 comments:
Post a Comment