Mbunge wa Jimbo la Mbozi Magharibi Mheshimiwa David Silinde.
*Dr Siyame kulipa gharama za kesi.
*Kesi yaondolewa kabla ya hukumu.
*Miaka mitatu ya ushindi.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Jopo
la majaji watatu wa mahakama ya Rufaa Mkoani Mbeya, wametupilia mbali
rufaa ya Mbunge wa zamani wa Jimbo la Magharibi kwa tiketi ya CCM Dr
Lucas Siyame ya kupinga matokeo ya Uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba
mwaka huu dhidi ya Mbunge wa sasa mheshimiwa David Silinde wa tiketi ya
CHADEMA.
Mheshimiwa
Silinde alitetewa na wakili wa kujitegemea Bwana Benjamin Mwakaganda na
Dr. Siyame alikuwa akitetewa na wakili Bwana Victor Mkumbe.
Kesi
hiyo ambayo imesikilizwa na jopo la Majaji wa tatu wa mahakama ya
rufaa, wakiongozwa na Jaji Msofe akisaidiana na Jaji Mbaruku.
Mapema
Mei 2 mwaka huu katika mahakama hiyo ambayo ni ngazi ya juu kabisa,
Wakili wa Dr. Siyame aliiambia mahakama kuwa wao kama walalamikaji
wameamua kuiondoa kesi na hawako tayari kuendelea nayo na kwamba wako
tayari kulipa gharama zote za kesi hiyo.
Awali
keeshi hiyo ilitolewa hukumu mahakama kuu Julai mosi mwaka 2011, ambapo
mahakama hiyo chini ya Jaji Wambura ilimpa ushindi Mbunge David
Silinde, hivyo kumlazimu Dr, Siyame kukata rufaabkupinga hukumu hiyo,
ambapo alidai kuwa Vituo vya kupigia kura vilizidishwa na pia kulikuwepo
na kura hewa ambazo zilimpa ushindi Silinde katika majumuisho ya kura
na pia fomu za matokeo hazikuwa halali.
Kesi
hiyo iliyodumu kwa muda wa miezi 10 na kuisha Mei 2 mwaka huu, ilivuta
watu wengi katika jengo la mahakama kuu Jijini Mbeya katika eneo la
Forest.
Mheshimiwa
Silinde kupitia wakili wake amesema ndani ya siku 60 wawe wamewasilisha
madai ya gharama za kesi hiyo ili ziweze kupitiwa na wakili wa Dr.
Siyame ili zilipwe.
Hata
hivyo akionge nje ya mahakama Mbunge huyo amesema huo ni ushindi wake
wa tatu mfululizo kupitia Uchaguzi mkuu ambapo Novemba 3 mwaka 2010
alitangazwa kuwa mshindi wa Jimbo la Mbozi Magharibi, na wa pili Julai
mosi 2011 aliposhinda mahakama kuu na watatu ni Mei 2 mwaka huu katika
mahakama ya rufaa na kuongeza kuwa kesi zote za CHADEMA zinazotolewa
maamuzi kati ya Mei 1 mpaka 5 lazima ishinde.
0 comments:
Post a Comment