Pages


Home » » UNYWAJI POMBE WA MWANAFUNZI AWAPO DARASANI WAMSABABISHIA KUFUKUZWA SHULE MKOANI MBEYA.

UNYWAJI POMBE WA MWANAFUNZI AWAPO DARASANI WAMSABABISHIA KUFUKUZWA SHULE MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 02:49 | 0 comments
Habari na Pulkeria Kisoka, Mbozi.
Mwanafunzi wa Kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Kutwa Mlowo, Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya Tabu Mfyeti, amefukuzwa shule baada ya kukutwa akinywa pombe darasani na wengine 9 wakiwa kwenye uchunguzi na maamuzi ya bodi.

Akiongea na mwandishi wetu Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Sufyan Msarilwa, amesema mwanafunzi huyo ni wa kike na alikutwa akinywa pombe na amekuwa akifanya hivyo mara kwa mara wakati wa masomo pamoja na wenzake hao 9 ambao wanaendelea kuchunguzwa.

Kwa upande wake mwanafunzi huyo Tabu amekiri kutenda kosa hilo na kwamba amekuwa akinywa pombe kwa madai ya kuwa hawezi kusoma bila kufanya hivyo.

Hata hivyo jitihada za wazazi wa mwanafunzi huyo kuuomba uongozi wa shule hiyo kumsamehe mtoto wao zimegonga mwamba kutokana na kile kilichotamkwa na uongozi huo kuwa wamechoshwa na tabia chafu za mwanafunzi huyo.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger