Pages


Home » » MKUU WA WILAYA ASAIDIA KUZIMA MOTO TREKTA LA MWEKEZAJI BAADA YA WANANCHI KULICHOMA MOTO.

MKUU WA WILAYA ASAIDIA KUZIMA MOTO TREKTA LA MWEKEZAJI BAADA YA WANANCHI KULICHOMA MOTO.

Kamanga na Matukio | 05:31 | 0 comments
Baadhi ya eneo ambalo Mwekezaji wa Kapunga Rice Project ameshindwa kuyalima na kuacha kama pori na kuwaacha wananchi wakiangaika kutokana na kukosa maeneo ya kulima, na waliolima mwekezaji awazuia kutochukua mazao yao.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Ramadhani Nyoni, akiwasihi vijana wasifanye vurugu.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mgogoro kati ya Mwekezaji wa Shamba la Kapunga Rice Project (KRP) na wananchi wa Kijiji cha Kapunga, Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, umeingia katika sura mpya baada ya watu wasiofahamika kulichoma Trekta la mwekezaji kwa moto.

Hata hivyo trekta hilo halikuteketea lote baada ya kufanikiwa kuwahi kuuzima ambapo hasara iliyopatikana kutokana na moto huo bado haijafahamika.

Mkuu wa wilaya hiyo Kanali Cosmas Kayombo ambaye amepata uhamisho na kuhamia wilaya mpya ya Kakonko kufuatia uteuzi wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JAKAYA KIKWETE, ameweza kutembelea eneo hilo la tukio ili kujionea hali ambayo imemsikitisha, ambapo alimuamuru dereva kupanda katika trekta hilo na kuliendesha kwa kasi katika mchanga ndipo moto ukazima.

Baada ya kuzikutanisha pande zote mbili baina ya Mwekezaji na wananchi wa kijiji hicho waliamua kusameheana na chanzo mgogoro huo kimetokana na kitendo cha mwekezaji kufunga njia zote hali iliyopelekea wananchi kushindwa kutoa mazao yao mashambani.

Hata hivyo baada ya kikao hicho mwekezaji aliruhusu njia moja ya kontena kutumika kwa kibali maalumu kutoka saa 1:30 asubuhi mpaka saa 11 jioni, ambapo pia wananchi walilalamikia kuwa njia hiyo ipo mbali hivyo inaleta kero.

Aidha wananchi hao ilitakiwa wafanye maandamano jana ilikufikisha ujumbe kwa Mkuu wa wilaya, lakini pia wamesikitishwa na hatua ya mkuu huyo wa wilaya kuhamishwa huku hajamaliza mgogoro huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho Ramadhani Nyoni amesema kuwa kitendo hicho ni kinyume cha Sheria na kwamba mipaka iliyowekwa na mwekezaji huyo inatokana na kuhofiwa kuibiwa mpunga na wananchi baada ya baadhi ya wananchi kuanza kuiba mpunga wake ukiwa shambani.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger