Tumefanikiwa kuangaza Vijijini na
kutembelea katika Shule ya Walemavu ka Katumba 2 iliyopo Wilaya ya
Rungwe, Mkoani Mbeya, jamani wanahitaji msaada ili naowajione wananafasi
na mchango mkubwa wenye umuhimu katika jamii,
Sio kuwatenga, sio kuwaacha kwani sote ni sawa, kumbuka kuwa nao wanandoto kuwa kama huyu na yule.
Saidia kwa moyo wako kwa watoto hawa.
Sote yatupasa kuwa nao, tushirikiane
kwa pamoja tuhakikishe nao pia wanapata elimu ya kutosha.(Picha na
Kamanga na Matukio & Chimbuko Letu, Katumba - Mbeya)
******
Makala na Ester Macha, Mbeya.
Walemavu ni watu ambao wanatakiwa kuthaminiwa
katika jamii
kutokana na hali halisi ya maumbile yao
waliyozaliwa nayo kuwa hivyo ,hakuna budi jamii hiyo ikapewa kipaumbele
katika masuala muhimun hususani suala la elimu ambapo wengi wao wamekuwa
nyuma kielimu.
Nadiriki kusema hivyo kwasababu mara nyingi jamii imekuwa
ikiwasahau walemavu na kuatenga kutokana na jinsi walivyo na kusahau kuwa nao
wana haki ya kuheshimiwa, kupendwa,kuthaminiwa kama
watu wengine ambavyo wanajaliwa na
jamii.
Lakini cha kushangaza hali hiyo imekuwa tofauti kwa jamii
hii ya walemavu ambapo baadhi ya kaya zimekuwa zikiwatenga watu hawa kwa
kuwafungia ndani kwa kuona kuwa ni mkosi katika familia husika.
Vile vile hata wabunge na madiwani wamekuwa wakisahau jukumu la kuwasaidia walemavu na kujikuta
wakiendelea kusaidia wananchi wengine huku wakifahamu kuwa kuna kundi lingine
la walemavu ambao wanahitaji msaada mkubwa hasa maeneo ya vijijini ambako
wamekuwa na dhana ya kuona kuwa walemavu ni mkosi katika familia zao.
Nashauri viongozi waliopewa mamlaka ya kusaidia wananchi pia
waone au kufika vijijini na kutambua kero mbali za walemavu na si kuwaangalia
watu wanaojiweza pekee yao
ambao ndio wameona ni msaada pekee kwao.
Huko vijijini kuna walemavu wapo ndani zaidi ya miaka 20
hawajawahi kutoka nje zaidi kukaa ndani tu,kama
viongozi hawataweza kujua kero za wapiga wao kwa kuangalia pande zote mbili
ambazo ni walemavu na wananchi wenye uwezo huku wakisahau kundi hili la
walemavu ambao nao ni wapiga kura licha ya kuwa ni walemavu.
Nionanavyo kwa wabunge
na madiwani wajaribu pia kuwapa kipaumbile walemavu wa aina zote kuliko
kuwasahau na kujikita zaidi na kundi moja tu ambalo ni wananchi ambao hawana
tatizo lolote katika viungo vyao.
Katika pita pita yangu nimekuwa nikishuhudia mikutano au
vikao vingi ambavyo vimekuwa vikifanywa na Wabunge na Madiwani lakini kilichonisahangaza sijaona kati ya
viongozi hawa aliyejaribu kukugusia kero za walemavu ambazo zinawakabili katika
maeneo yao.
Jambo ambalo nimeliona na ambalo linatakiwa kuigwa na
wabunge na madiwani wengine ni hili la
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw.Philipo Mulugo (Mb)kuweka
kipaumbele kwa walemavu na wazee ambao hawajiwezi kimaisha kuwasaidia kila
anapofika kufanya mikutano ya hadhara katika Jimbo hilo yote ni kuweza kujua kero za wananchi wote.
Nimemua kusema hivi si kwamba nimeamua kumpa sifa Mbunge
huyu bali ni kutokana na utendaji wa kazi yake ya Ubunge ambao amekuwa
akiufanya bila ubaguzi kwa kuona kuwa kuwa kundi maalumu la walemavu wote ambao
wanastahili kupata huduma na kama watu
wengine.
Kwa kutambua kundi hili mbalo mara nyingi limekuwa
likitengwa na jamii na hata wengine
wameshindwa kutoka ndani zaidi ya miaka
20 sasa Bw.Mulugo aliamua kutoa baiskeli 200
zenye thamani ya mil.50 kwa walemavu na wazee wote wa jimbo la Songwe .
Ninachokiona hapa ni kwamba
Mbunge huyu aliamua kufanya hivi baada ya kuona kuwa jimbo hilo la
Songwe kuwa na idadi kubwa ya walemavu ambao hawakuw na msaada wowote na kuona
umuhimu wa kuwasaidia wale walemavu ambao hawajaweza kutoka ndani kwa muda
mrefu kutokana na hali halisi waliyonayo.
Si jimbo la songwe pekee lenye walemavu bali hata Jimbo la
Mbeya lina walemavu wengi ambao wanahitaji vitendea kazi ili waweze kutembea na
kufanya shughuli zao je nani wa kuwaona kama
si viongozi wenyewe kuangalia makundi haya ambayo mara kadhaa yamekuwa yakitengwa na jamii?
Nimekuwa nikishuhudia idadi kubwa ya walemavu wakiwa mitaani
kuomba kuomba ili kuweza kujikimu kimaisha kutokana na hali duni waliyonayo ya
kimaisha.
Ifike wakati viongozi wetu waliopewa mamlaka ya kusaidia
wapiga kura waweke kipaumbele suala hili hata kwa kuwapatia mitaji ya biashara
ili waweze kuendesha maisha yao
kuliko kutegemea kupewa fedha kidogo ambazo haziwafikishi popote zaidi ya
kuwaongezea ugumu wa maisha.
Sawa hata hili wazo la Mbunge wa Jimbo la Songwe la
kuwasaidia baiskeli si baya kwani kuna
wengine ambao hawajiwezi kabisa kutembea kufika saehemu nyingine kujitafutia
riziki hii nayo itakuwa msaada mkubwa kwao.
Nionavyo kwa upeo wangu msaada huu hautoshi pekee bali
kinachotakiwa ni kupata nguvu nyingine ya kuwasaidia walemavu ili nao waweze kujisaidia wenyewe kwa nguvu
zao kwa kuwa wamepata vifaa mbavyo vitawawezesha kuweza kushiriki vema shughuli
zote za kijamii.
Si kwamba napinga msaada wa Bw. Mulugo kwanza napongeza kw
wazo zuri alilokaa na kufikiri kwamba kundi hili limekuwa likihitaji msaada
mkubwa na pia ameona mbali kwa kuona kuwa walemavu mara nyingi ni watu ambao
wanakuwa watengwa na jamii na hata viongozi waliowengi wamekuwa wakiwasahau kwa
mchango wao.
Ushauri wangu kwa Bw.Mulugo ni kuongeza bidii zaidi kwa
kutafuta mbinu mbali mbali za kuweza kuwsaidia walemavu wa jimbo lake ambao kwa
sasa wamepata miguu ya kutembelea kikubwa kilichopo kwao ni Mbunge huyu kuwatafutia mitaji ili wawez kufanya shughuli zao wenyewe na si kukaa kutegemea
kupata misaada.
Tatizo ni kwamba wabunge na madiwani walio waliowengi hawana
tabia ya kuongelea masuala ya walemavu badala yake wamekuwa wakijikita zaidi
kwa watu wa kundi moja tu na kusahau kuwa kundi la walemavu ni muhimu pia
kulisaidia.
Wabunge wengine na madiwani igeni mfano wa Naibu Waziri wa
Elimu ambaye kwa kiasi kikubwa ndiye amekuwa akijali zaidi kundi hili la walemavu
kuliko wabunge wengine ambao wamekuwa
wakijali zaidi makundi mengine na kusahau kundi la walemavu.
Si kwamba wabunge hawa wengine wamekuwa hawaombi misaada kwa
wahisani kusaidia wananchi wao lakini wanachokifanya wao misaada hiyo inaishia
kwenye shughuli zao binafsi badala ya kukumbuka na wananchi waliomfanya akawa
mbunge.
Na hata Bw. Mulugo pia amekuwa akikumbuka fadhila ambayo
amefanyiwa na wananchi wake na kukumbuka kile anachopata kuwapatia wapiga kura
wake hata kama kidogo.
Ni kwamba misaada pekee haitoshi bali kitu kingine cha
muhimu kinahitajika ni kuisaidia jamii hii iweze kupata elimu kwani walemavu
wengine wana uwezo mkubwa wa kielimu lakini tatizo ni jinsi ya kufikia maeneo ya shule kutokana na hali halisi ya maumbile waliyonayo.
Mbunge huyu mpango wake wa kusaidia walemavu ni mzuri lakini
pia azidi kuboresha suala la elimu kwani kuna walemavu wengine bado wanahitaji
zaidi kusoma misaada pekee haitoshi kwani watasaidiwa mpaka lini?
Lakini pia nimshukuru Bw.Mulugo kwa kufikiri mbali na kuona
kuwa kuna haja ya kusaidia kundi hilo ambalo wabunge wengine hawajaweza
kusaidia au hata kuuliza majimbo yao yana
walemavu wangapi,lakini Mbunge huyu awe mfano kwa kujali walemavu na
wabunge wengine na madiwani waige mfano huu.
Kwa mpango huu utawafanya wabunge wote waonekane kujali
makundi yote na si kubagua kama ilivyo kwa
wabunge wengine kinachotakiwa kwa wao ni kuona umuhimu wa kusaidia makundi yote
katika jamii na si kuangalia nafasi ya mtu katika jamii.
Sidhani kama kuna
wbunge wenye mawazo ya kusaidia kundi
hili wengi wa viongozi akifika kufanya mikutano yake hana haja ya kuuliza kama kuna kundi la walemavu katika Jimbo lake
hili linatakiwa kuanza kufanyika kwa kufuata mfano wa Mbunge wa Jimbo la Songwe
ambaye ameanza kuonyesha njia kwa wabunge wenzake kuwa kunma umuhimu wa
kusaidia kundi hilo.
Ninachotaka kushauri ni kuwa
wabunge na madiwani waweke kipaumbele makundi ya walemavu wa aina zote
pale wanapotembelea majimbo yao na kufanya mikutano wawe na ajenda ya
kuzungumzia masuala ya walemavu kwa kutambua kero mbali mbali ambazo
zinawakabili katika maeneo yao kwani kuna wazazi wengine wamewaficha walemavu
ndani kwa kuogopa aibu kwa jamii.
Ili hili lisiendelee kuna
haja kwa viongozi kufanya haya ili walemavu waliofichwa majumbani waweze kutolewa
nje na kusaidiwa kwa kufanya hivyo
kutafanya idadi ya walemavu wanaofichwa ndani kupungua na hata wale ambao
walikuwa hawatembei wataanza kujishughulisha ili kujiongezea vipato na hatimaye kuacha kuwa tegemezi.
0 comments:
Post a Comment