Waziri Mkuu Mheshimiwa Pinda akiwa
ameongozana na viongozi wa sekta mbalimbali wakiwemo wabonge, Mkuu wa
mkoa na wengineo, katika Kiwanda cha kusindika nyama Jijini Mbeya.
******
Habari na Mwanishi wetu..
Kiwanda cha kusindika nyama kilichopo Mkoani Mbeya
kilichotelekezwa na serikali kwa zaidi ya miaka 30 sasa kimepata matumaini ya
kufufuka baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kukitembelea na kutoa maagizo.
Katika maagizo yake Waziri mkuu Pinda amelitaka
Shirika hodhi la Mashirika ya umma nchini (CHC) kuhakikisha viwanda viwili vya
nyama vya Tanganyika Parkers vilivyopo katika mikoa ya Mbeya na Shinyanga
vinapata wawekezaji kabla ya mwezi Desemba mwaka huu.
Aidha ametaka viwanda vinavyohusiana na usindikaji
wa mazao ya wakulima ndivyo vipewe kipaumbele ili wananchi wa kawaida waweze
kunufaika kutokana na vijana kupata ajira.
Awali, akisoma taarifa ya kiwanda hicho, Afisa wa
Tanganika Parkers, Joseph Mapunda amesema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho ulianza
mwaka 1975 na ulipaswa kukamilika na kuanza kazi mwaka 1985.
Hata hivyo amesema kuwa ujenzi huo ulisimama mwaka
1978 kutokana na ukosefu wa fedha pamoja na taifa wakati huo kuingia vitani
dhidi ya nduli Idd Amini wa Uganda.
0 comments:
Post a Comment