Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda
akiongea na wananchi pamoja na wafanyakazi wa Kiwanda cha Marumaru,
Jijini Mbeya jana wakati wa ziara yake ya siku tatu.
*******
Habari na Mwandishi wetu.
Waziri
Mkuu, Mizengo Peter Pinda amewasili mkoani Mbeya kwa ziara ya siku tatu ambapo
baada ya kupokea taarifa ya mkoa alisema kuwa suala la uuzaji wa kahawa mbichi
liachwe mikononi kwa wakulima wenyewe kutokana na kwamba hasara na faida ya zao
hilo ipo juu yao.
Aidha
Pinda amesema kuwa suala la ujenzi wa miundombinu kwa mkoa wa Mbeya
linaangaliwa kwa umakini zaidi ambapo ujenzi wa uwanja wa ndege unatarajia
kukamilika hivi pundu kutokana na serikali kuwa na imani kuwa kukamilika kwake
kutauwezesha mkoa kupiga hatua katika nyanja mbalimbali ikiwemo kilimo.
Akiwa
katika kiwanda cha nyama cha Tanganyika Pekers kilichopo katika kata ya
utengule Usonge wilaya Mbeya vijijini waziri mkuu Pinda amesema kukamilika kwa
kiwanda hicho kutawezesha ajira kwa zaidi ya vijana 2000 na kuongeza kuwa
kukosekana kwa mwekezaji wa kiwanda hicho kumechangia kuchelewa kwa utendaji
kazi wa kiwanda hicho.
Wakati
huohuo wamewataka wamiliki wa vindanda vya kusindika nyama na mazao mbalimbali
kuwatumia wakulima na wafugaji wadogo ili waweze kunufaika kupitia shughuli
zao.
0 comments:
Post a Comment