Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mwalimu Lawrence Katindasa wa Shule
ya Msingi Mtumbo - Ilembo, Kata ya Vwawa, Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya,
ametuhumiwa kuuza mbao 241 mali ya shule hiyo.
Mwalimu mkuu huyo alipewa jukumu la
kusimamia upasuaji wa mbao hizo na Kamati ya shule chini ya Mwenyekiti
Tuya, na mara baada ya kukamilika kupasuliwa zitumike katika ukarabati
wa shule hiyo, lakini mwalimu alikiuka na kuwauzia mafundi waliokuwa
wakizipasua na pesa zote kuzitumia kwa maslahi yake.
Wapasuaji mbao hao walikamatwa na
Mwenyekiti huyo wa kamati ya shule ambaye aliwapeleka kwa Afisa mtendaji
wa mtaa Bwana Ally Nzowa, ambaye naye aliwapeleka Kituo cha Polisi.
Aidha, Mwalimu Katindasa alipoitwa
alikiri kuwauzia wapasua mbao hao mbao 241 na baadae Polisi hao
waliamuru suala hilo likamalizwe shuleni kwa kuwa mwalimu amekiri kosa
na walipewa mbao hizo walidai kuwa ni malipo kutokana na kazi waliyokuwa
wanaifanya shuleni hapo.
Baada ya kutoka polisi mafundi hao
waligoma kuzirejesha mbao hizo shuleni kwa madai wamepewa na mwalimu
mkuu huyo, lakini Mwalimu huyo alikiri atazirejesha baada ya wiki moja
toka alipotakiwa kufanya hivyo Novemba 2011, lakini baada ya muda huo
kufikana yeye kusindwa kuwasilisha mbao hizo aliomba aongezewe muda
yaani mwishoni mwa mwezi Novemba.
Lakini hata hivyo alishindwa kufanya hivyo licha ya kuombwa mara kwa mara na kamati ya shule.
Baadhi ya wajumbe walipomtaka Mwalimu
Mkuu Katindasa kuahidi ni lini atalipa walisema kuwa mwalimu huyo ni
mhehe hivyo ana hasira anaweza kujinyonga na kwa upande wake kudai kuwa
anaomba asifuatiliwe mara kwa mara na mpaka sasa anaumwa.
Suala hilo lilifuatiliwa na Afisa
mtendaji Bwana Nzowa ambaye amesema atalifikisha polisiili wale wote
waliohusika na ufujaji wa mbao hizo wachukuliwe hatua za kisheria.
Hata
hivyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mei 7 mwaka huu, mtaani
hapo wananchi walikasirishwa na kitendo cha mwalimu huyo kutokana na
hujuma huku alifahamu dhahiri kufanya hivyo ni kosa kutokana na
kuaminiwa.
0 comments:
Post a Comment