Na Bosco Nyambege ,Rujewa
Umoja wa Wanawake kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi
katika Ushirika wa Yerusalemu iliyopo Mkoani Mbeya wamezuru Gereza
la Rujewa iliyopo Wilayani Mbarali hivi karibuni.
Ziara hiyo iliambatana na kutoa zawadi kwawafungwa wote wa Gereza
hilo kama katoni nane za sabuni,mafuta ya kujipaka yaani lotion na
mafuta ya mgando dazani 40 ikiwa pamoja na chumvi .
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake ushirika wa yerusalemu Eda Kapora
alipohojiwa kuhusiana na suala hilo alidai kuwa hiyo ni moja ya huduma
wanayofanya wanawake amabyo ni dhamana ya mzigo wa liopewa na mwenyezi
mungu wa kutembelea wajane ikiwa pamoja na wafungwa ,watoto yatima na
watu wanaoishi katika mazingira magumu .
Kapora aliongeza kuwa kwani mpaka sasa wamekwisha kutembelea vituo
mbalimbali kama vile watoto yatima ,nyumba za wajane watu wanaoishi
ktika mazingira magumu n a ka sasa wameanza kuzuru katika magereza .
Kwa upande wake mchungaji mlezi wa kanisa hilo Peter Mwambalaswa
alisema kuwa dini iliyo safi n kutazama wafungwa ,wajane na wanaoishi
katika mazingira magumu .
Hata hivyo alisema kuwa ni muhimu kwa kanisa lolote kutambua wajibu
mkubwa waliopewa na mwenyezi mungu juu ya kuhudumia wale wanaowazunguka
na wale walio mbali nao wanaohitaji msaada wao .
Vilevle alsema kuwa ni vyema askari magereza wanaofanya kazi ya
kuwalinda wafungwa magerezani kutambua kwama wao ni wachungaji na mungu
atawalipa kama watafanya yale wanaompendeza yeye .
Alison Mwasile ambaye ni mchungaji wakanisa la Moravian Usharika
wa Rujewa amewasihi wafungwa kuonesha ushirikiano wao mzuri baina yao
na mungu pindi wanapokuwa gerezani na pindi wanapokuwa wanatoka .
Mwasile alisema kuwa magerezani wapo walimu wazuri wa imanikwani
hata kipindi cha yusufu alipfunga gerezani kuilikuwa na kusudi maalumu
ambalo mungu aliliweka ndani yake .
Mmoja wa wafungwa amabaye jina lake hakutaka jina lake litajwe
aliyaomba makanisa na dini mbalimbali kuweza kuwaombea kwani wapo
walio magerezani hawana hatia yeyote .
Kwa upande wake Askari wa Gereza hilo ambaye jina lake hakutaka
litajwe katika gazeti hili alisema ujio wa makanisa gerezani
kunapelekea wao kuona mwanga katia maisha yao kwani wanapata mawazo
mbalimbali kutoka kwa watumishi wa mungu kuhusiana na shughuli zao..
Alisema kuwa hata kwa upande wa wafungwa ni furaha kubwa kuona
watumishi wa mungu wanaokuja kuwatembelea maeneo hayo kwani wanapata
faraja na matumani katika maisha yao hata wawapo gerezani .
0 comments:
Post a Comment