Pages


Home » » HABARI MPASUKO!!!MKUU WA WILAYA YA MBOZI AJIUZULU

HABARI MPASUKO!!!MKUU WA WILAYA YA MBOZI AJIUZULU

Kamanga na Matukio | 02:21 | 0 comments
WAZIRI WA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA PROFESA JUMANNE MAGHEMBE AMEELEZWA KUSABABISHA MKUU WA WILAYA YA MBOZI BW.GABRIEL KIMOLO KUJIUZULU WADHIFA WAKE WA MKUU WA WILAYA KUTOKANA NA KITENDO CHAKE CHA KUENDELEA KUKUMBATIA  BAADHI YA WAFANYABIASHARA WANUNUZI WA KAHAWA AMBAO WAMEKUWA WAKISEMA KWAMBA HAWAZUNGUMZI NA MBWA  BALI WANAZUNGUMZA NA MFUGA MBWA.
 
KUJIUZULU KWA BW.KIMOLO AMBAYE AMEKUWA NI MKUU WA WILAYA YA KWANZA NCHINI KUAMUA KUACHIA WADHIFA HUO KWA KIPINDI CHA ZAIDI YA MIAKA 20 KWA AWAMU ZA UONGOZI WA SERIKALI YA CHAMA TAWALA KUMESABABISHWA NA SABABU ALIZOELEZA KUWA AMEKOSA USHIRIKIANO NA WIZARA YA KILIMO KUHUSU MSIMAMO WAKE WA KUPINGA UNUNUZI WA KAHAWA MBIVU RED CHERY AMBAYO INAFANYWA NA BAADHI YA WAFANYABIASHARA WANAOPATA RIDHAA YA KUNUNUA KUTOKA WIZARANI.
JANUARI 17 MWAKA HUU WAZIRI WA KILIMO NA USHIRIKA PROFESA MAGHEMBE ALIKUTANA NA BAADHI YA WAKULIMA NA WADAU WA ZAO LA KAHAWA AMBAPO MSIMAMO WA SERIKALI ULIELEZA KUWA HAWAKO TAYARI KUENDELEA KUWAONA WAKULIMA WAKIUZA KAHAWA MBICHI KWA WACHUUZI HALI AMBAYO BW. KIMOLO ALISEMA IMESABABISHA YEYE KUONEKANA KUTOTHAMINIWA MSIMAMO WAKE NA WA SERIKALI YA WILAYA YA MKOA.
 
KADHALIKA KATIKA MAELEZO YAKE YA KUJIUZULU BW.KIMOLO ALISEMA KUWA KWA MUJIBU WA UTARATIBU WA UTEUZI WA UNAOFANYWA NA RAIS YEYE UTEUZI WAKE ULIANZIA MWAKA 2006 NA KUKOMA MWAKA 2010 AMBAPO HADI SASA HAKUNA UTEUZI MPYA ULIOFANYWA NA RAIS JAMBO LINALOMFANYA ASHINDWE KUPANGA MIKAKATI YA KAZI KWA MAENDELEO YA WILAYA YAKE.
 
ALISEMA KUWA, HIVI SASA NI MWAKA MMOJA NA NUSU AMEKUWA AKIFANYA KAZI KWA MATUKIO YA DHARURA NA MAAGIZO KUTOKA JUU NA HIVYO KUMFANYA AONEKANE KUTOWAJIBIKA VILIVYO KATIKA NAFASI YAKE NA KWAMBA AMEAMUA KUJIUZULU AKIAMINI KUWA UAMUZI WAKE UTALINDA HESHIMA YAKE.
AIDHA AINAELEZWA KUWA BW.KIMOLO AMEKUWA NI MTU WA KARIBU SANA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU BW. EDWARD LOWASSA NA KWAMBA KITENDO CHAKE CHA KUJIUZULU KINA BARAKA KUTOKA KWA KIONGOZI HUYO MSTAAFU AMBAPO KATIKA ZIARA YAKE ALIYOIFANYA HIVI KARIBUNI WILAYANI MOMBA KATIKA MJI MDOGO WA TUNDUMA ALITETA NAYE JAMBO MUHIMU.

HATA HIVYO TETESI ZA KUTOKUWEMO KATIKA UTEUZI UJAO ZINAELEZWA KUWA NI MOJA YA SABABU ZILIZOMFANYA MKUU HUYO KUACHIA NGAZI MAPEMA ILI KUJIJENGEA MAZINGIRA YA MAANDALIZI YA KUIKUBALI HALI HIYO KABLA HAIJATOKEA WAKATI WA UTEUZI AMBAO UNATARAJIWA KUFANYWA NA RAIS WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA.
 
ALIFAFANUA KUWA KUMEKUWA NA UBABAISHAJI KWA BAADHI YA VIONGOZI NA KUSABABISHA SERIKALI IONEKANE INASHINDWA KUWATUMIKIA VYEMA WANANCHI NA KWAMBA YEYE AMEAMUA KUACHIA NGAZI NA ANAKWENDA KUSHUGHULIKIA MAMBO YAKE BINAFSI.
 
ALIPOTAKIWA KUELEZA KAMA DHAMIRA YAKE ITAJIKITA ZAIDI KATIKA SIASA ALISEMA KUWA WAKATI UKIFIKA KUINGIA KATIKA MCHAKATO WA KISIASA ATAFANYA HIVYO KWA KUWA YEYE KAMA MTU YEYOTE ANA UAMUZI WAKE.
 
‘’NIMECHOSHWA NA KEJELI NA MIZENGWE DHIDI YA SERIKALI..WAFANYABIASHARA WANADILIKI KUSEMA KUWA HAWAKO TAYARI KUZUNGUMZA NA MBWA BALI WANAZUNGUMZA NA WENYE MBWA, SIWEZI KUFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA YA AINA HII, WANANCHI WAELEWE HIVYO,NITABAKI KUWA RAIA MWEMA NA MWANANCHI WA KAWAIDA KAMA WENGINE.’’ALISEMA BW.KIMOLO.
 
ALIFAFANUA KUWA AMEMUANDIKIA BARUA RAIS, WAZIRI MKUU NA MKUU WA MKOA WA MBEYA KUMJULISHA HILO NA KWAMBA HUO NI UAMUZI WAKE BINAFSI NA JIBU LOLOTE HALITABADILI UAMUZI WAKE ALIOAMUA KUUCHUKUA.
 
KABLA YA KUCHUKUA UAMUZI HUO BWANA KIMOLO ALIHUDHURIA BARAZA LA USHAURI WA MKOA (RCC), KATIKA UKUMBI WA MKAPA MAPEMA MEI 4 MWAKA HUU NA KUTOA MCHANGO MKUBWA JUU YA UANZISHWAJI WA BENKI YA WANANCHI WILAYA YA MBOZI NA KUPONGEZWA NA MWENYEKITI WA MKUTANO HUO BWANA ABAS KANDORO, AMBAYE PIA NI MKUU WA MKOA WA MBEYA. 

HATA HIVYO AMENUSURIKA KATIKA AJALI YA BARABARANI ENEO LA MLOWO ALIPOKUWA KATIKA HARAKATI HIZO ZA KUJIUZULU KWAKE, NA MARA KADHHA ALIONEKANA AKITETA NA MKUU WA MKOA KABLA YA KUBEBA VITABU VYAKE NA KUONDOKA MAJIRA YA SAA SITA MCHANA.

BWANA KIMOLO AMESEMA TAARIFA KAMILI ZA KUJIUZULU KWAKE ATAITOA MEI 5 MWAKA HUU KATIKA OFISI ZA MKUU WA WILAYA MBOZI.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger