Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Wanafunzi
wa Shule mbili za msingi Ilembo na Mtumbo, Kata ya Vwawa, wilaya ya
Mbozi, mkoani Mbeya wamelazimika kujisaidia haza ndogo na kubwa porini
na mashambani kutokana na vyoo vya shule hizo kujaa kwa zaidi ya mwaka
mmoja.
Hayo
yamebainika baada ya kutembelea shule hizo mbili na kukuta maandamano
makubwa kwa majirani waliopo mita chache kutoka shuleni hizo, huku
baadhi ya wanafunzi wakipokea matusi na wengine kufukuzwa na majirani
hao.
Wingi wa
wanafunzi wanaosoma katika shule hizo wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa
huku wazazi wa vitongoji sita vinavyozunguka shule hizo, wamekuwa katika
marumbano kwa takribani mwaka mmoja kutokana na baadhi kuchangia
mchango wa shilingi 2,000 kwa kipindi chote bila sababu ya msingi.
Afisa
mtendaji wa mtaa wa Ilembo Bwana Ally Nzowa amesema kati ya wananchi
4,442 waliotakiwa kuchangia fesha hizo shilingi 8,884,000 ni watu 592
wamechangia shilingi 1,184,000 hivyo kukwamisha kabisa shughuli za
ujenzi wa vyoo hivyo na kati ya pesa hizo shilingi 43,500 zimetumika na
salio halisi ni shilingi 1,140,500.
Hata
hivyo Mtendaji huyo amebainisha kuwa wazazi wa mitaa ipatayo saba
wamekosa moyo wa uzalendo kwa kuchangia pesa ambayo ni mitaa ya Kitovuni
A, Kitovuni B, Matengu A, Matengu B, Majengo, Nsenya na Namleya.
Mkuutano
huyo uliofanyika katika mtaani hapo na kusimamiwa na Mwenyekiti wa mtaa
wa Ilembo B, Bwana Henry Singogo amewataka wazazi kulipa michango hiyo
ifikapo mwishoni mwa mwezi Mei ili kukamilisha ujenzi wa vyoo hivyo.
Hata
hivyo waliazimia yeyote atakayekaidi kuchangia pesa hizo achukuliwa
hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfikisha mahakamani kwa
kukwamisha maendeleo.
0 comments:
Post a Comment