Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bwana Abbas
Kandoro akipokea tunzo yake kutoka kwa Mwenyekiti wa Mbeya Press Club
Bwana Christopher Nyenyembe kutokana na ushirikiano anaoutoa kwa
waandishi wa habari mkoani hapa katika Ukumbi wa Itemba Village wakati
wa Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya habari duniani ambalo hufanyika kila
mwaka Mei 3.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bwana Abbas Kandoro akimkabidhi tunzo yake, Mwandishi
wa Gazeti la Raia mwema Bwana Felix Mwakyembe iliyotolewa na Chama wa
waandishi wa habari Mbeya Press Club, baada ya kushinda tunzo za Taifa
zinazotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bwana Abbas Kandoro akimkabidhi tunzo yake, Mwandishi
wa Gazeti la Tanzania daima na mmiliki wa Blogu ya Kalulunga Bwana Gordon Kalulunga, iliyotolewa na Chama wa
waandishi wa habari Mbeya Press Club, baada ya kushinda tunzo za Taifa
zinazotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bwana Abbas Kandoro akimkabidhi tunzo yake, Mwandishi
wa Gazeti la Majira Bi Esther Macha iliyotolewa na Chama wa
waandishi wa habari Mbeya Press Club, baada ya kushinda tunzo za Taifa
zinazotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bwana Abbas Kandoro akimkabidhi tunzo yake, Mwandishi
wa Bomba FM na mmiliki wa Blogu ya Kamanga na Matukio Bwana Ezekiel Kamanga iliyotolewa na Chama wa
waandishi wa habari Mbeya Press Club, baada ya kushinda tunzo za Taifa
zinazotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bwana Abbas
Kandoro akimkabidhi tunzo yake, Mwandishi wa Gazeti la Majira Bwana
Rashid Mkwinda iliyotolewa na Chama wa waandishi wa habari Mbeya Press
Club, baada ya kushinda tunzo za Taifa zinazotolewa na Baraza la Habari
Tanzania (MCT).
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa
Abbas Kandoro katika picha ya pamoja na Waandishi wa habari mkoani
Mbeya, nje ya Ukumbi wa Itemba Village mara baada ya kumalizika kwa
Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya habari.(Picha na Mbeya Yetu).
********
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya mheshimiwa Abbas Kandoro ameipongeza tasnia ya habari
mkoani hapa kwa mchango mkubwa katika uhabarishaji na uelishaji jamii.
Ameyasema
hayo katika Kongamano la siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari duniani,
ambapo kimkoa sherehe hizo zimefanyika katika Ukumbi wa Itemba Village
uliopo mtaa wa Veta jijini Mbeya Mei 3 mwaka huu.
Kandoro
amewaasa wamiliki wa vyombo vya habari kuwawezesha waandishi wa vyombo
vyao ili wananchi waweze kupata habari sahihi na kwa wakati muafaka,
lakini alitumia fursa hiyo kuwaonya waandhishi wa habari wasifanye kazi
yao kwa vitisho ili kuleta usawa katika jamii, kutokana na baadhi yao
wamekuwa wakiwatisha baadhi ya wananchi wanaodhani wanatuhuma.
Aidha
Mkuu huyo wa Mkoa Mheshimiwa Kandoro, amesema waandishi wa habari
wasiridhike hapo walipo bali wajiendeleze kielimu ili kukuza fani hiyo.
Naye,
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa Christopher Nyenyembe,
alimpongeza mkuu wa mkoa kwa ushirikiano anaoutoa kwa vyombo vya habari
hali inayofanya kazi ya uandishi kuwa rahisi na wananchi kupata habari
za uhakika.
Hata
hivyo Bwana Nyenyembe alichukua fursa ya kumkabidhi Mkuu wa Mkoa cheti
utumishi uliotukuka kutokana na mkuu huyo kuthamini mchango unaotolewa
na vyombo vya habari mkoani hapa.
Katika
kongamano hilo Nyenyembe alimuomba Mheshimiwa Kandoro kukabidhi vyeti
kwa waandishi mahili wanane waliopata tunzo za uandishi bora nchini
zilizotolewa na Baraza la habari Nchini (MCT).
Waandishi
wa habari waliokabidhiwa vyeti na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mheshimiwa
Kandoro ni pamoja na Esther Macha, Gordon Kalulunga, Keneth Mwazembe,
Festo Sikagonamo, Ezekiel Kamanga, Felix Mwakyembe, Christopher
Nyenyembe na Rashid Mkwinda.
Kwa
kutumia mchango wa waandishi wa habari hao na kuleta heshima kubwa kwa
mkoa mheshimiwa Kandoro, amesema atatoa shilingi laki moja kwa kila
mwandishi ili iwe chachu kwa wengine ili kufanya kazi kwa weledi mkubwa
na hivyo kuongeza juhudi katika tasnia nzima ya habari mkoani hapa.
0 comments:
Post a Comment