Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la
Ayoub Mwamboma mkazi wa Sinza, Wilaya ya Chunya, Mkoani Mbeya amefariki
dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba aina ya manila nje ya nyumba
ya mjomba wake mita chache kutoka nyumbani kwake.
Marehemu alikuwa muuza vinywaji
baridi katika Depot ya Bwana Nestory Ndelwa, ambaye ni wakala wa Kampuni
ya Cocacola ambapo alidaiwa kuhusika na upotevu wa pesa za mwajiri
wake.
Mei 6 mwaka huu mwajiri huyo alikuwa
na kikao na marehemu pamoja na ndugu zake na kudai ameingia hasara ya
shilingi 2,000,000 hali ambayo marehemu alikanusha na kwamba mwajiri
alimtaka kulipa shilingi 50,000 kila mwezi jambo ambalo alilikataa.
Mara baada ya kikao hicho Bwana Ndelwa alimwambia kuwa marehemu atampeleka Polisi Mei 7 mwaka huu ili amfikishe mahakamani.
Uchunguzi umebaini baada ya kauli
hiyo na kikao kumalizika marehemu alighadhabika na kuchukua jukumu la
kujinyonga kwenye mti uliopo nje ya nyumba ya mjomba wake Bwana Leonard
Mwamboma, kutokana na baadhi ya watu aliowakopesha kreti zaidi ya 131
kukataa kumlipa(jina limehifadhiwa) na kwamba baada ya kushawishiwa
mudaiwa alidai angelipa kreti 35 mei 7 .
Aidha Polisi walifika eneo la tukio
kwa kuchelewa kutokana na kutumia muda wa masaa 4 kwa kilometa 50 licha
ya kupewa taarifa toka saa 12 asubuhi na kuuchukua mwili wa marehemu kwa
ajili ya uchunguzi na mara baada ya kukamilika mwili ulikabidhiwa kwa
ndugu zake kwa ajili ya kuufanyia mazishi katika makaburi ya Kibaoni
wilayani humo.
Hata hivyo katika uhai wake marehemu
ameshawahi kuwa mchezaji wa mpira wa miguu kupitia timu ya Itewe City na
Leopard zote za Wilaya ya Chunya kwa nyakati tofauti.
0 comments:
Post a Comment