*Baba yake afukuzwa kijijini kwa tuhuma za wizi
*Marehemu alituhumiwa kuiteketeza kwa moto Mahakama ya mwanzo.
******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mkazi mmoja wa Kijiji cha Igoma, Kata
ya Igoma, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoani Mbeya Riziki Limbakisya
(25), ameuawa na wananchi wenye hasira kali kwa tuhuma za wizi.
Tukio hilo limetokea Mei 15 mwaka huu
majira ya saa 11:25 jioni katika eneo la msitu wa Shule ya Sekondari
Igoma iliyopo wilayani humo, baada ya marehemu kukutwa akiwa na spika
na deck mali ya Bwana Elias Mbwete na Musa Mchona, ambavyo viliibiwa
katika nyakati tofauti kijijini hapo ambapo baada ya uchunguzi wahanga
walimbaini mtuhumiwa wao.
Kutokana na kuchoshwa na vitendo vya
wizi wa mara kwa mara kijijini hapo na mara baada ya kumkamata
walimpiga na kumsababishia majeraha mbalimbali mwilini mwake, ambapo
hasira zake ziliishia kwa kumteketeza baada ya kumzinga kwa shehena la
kuni zilizowashwa kwa petroli huku wananchi hao wakiimba nyimbo za
kejeli.
Baada ya tukio hilo uliitishwa
mkutano wa hadhara uliokuwa ukijadili masuala ya maendeleo ya kijiji
hicho, baada ya wananchi kumtaarifu Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bwana
Elias Mwaipopo ambapo wananchi wote walikimbilia eneo la tukio na
kukuta mwili wa marehemu ukiendelea kuteketea.
Naye, Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho
Bwana Samwel Malesa, baada ya kufika eneo la tukio alitoa taarifa kwa
Jeshi la Polisi, ambao walifika eneo la kijiji na kukuta baadhi ya mwili
wa marehemu ukiendelea kuteketea huku mikono yto ikiwa imeteketea
kabisa.
Kwa upande wake Bwana Elias Mbwete
alisema kuwa usiku wa Mei 14 mwaka huu Grocery yake ilivunjwa na kuibiwa
TV, Deck, remote 2, simu moja na pesa taslimu shilingi 145,000, hivyo
kufanya jumla ya mali zote zilizoibiwa kuwa na jumla ya thamani ya
shilingi 675,000.
Hata hivyo Mchungaji Abel Mwakisyala
wa Kanisa la Church Gospel International (COG) la kijiji hicho,
amesikitishwa sana na kitendo cha wananchi kujichukulia sheria mkononi,
lakini alivitaka vyombo vinavyosimamia sheria kufanya kazi kwa uadilifu
kwani wananchi hao huchoshwa na vitendo vya kuwaona wahalifu mitaani
pindi wanapokamatwa na makosa mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment