Habari na Ezekiel Kamanga, Rungwe.
Mkazi
wa Kijiji cha Mwela, Kata ya Kandete, Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya,
Bwana Chepe Mwasandube (50) ameamriwa kula udongo uliotumiwa kufukia
kaburi la marehemu Sion Mwajungwa (52) Aprili 28 mwaka huu.
Akiongea
na mwandishi wetu Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bwana Anania Mwakitenga,
amesema kuwa Bwana Mwasandube alituhumiwa kuwa ndiye aliyesababisha kifo
cha marehemu huyo kilichotokea Aprili 27 mwaka huu kijijini hapo.
Wanakijiji
walifika hatua hiyo baada ya mtuhumiwa huyo kutoonekana masibani baada
ya marehemu kufariki, ndipo walipoamua kumuita eneo la makaburi kisha
kumuamuru kula udongo ulio juu ya kaburi hilo na baadae walimpa pombe
kwa ajili ya kushushia udongo huo aliokula.
Baada
ya kumaliza kufanya hivyo aliambiwa adhabu yake imekwisha na yupo huru
na kumtaka asirudie tena kufanya vitendo vya kishirikina kama hivyo.
Aidha
baadhi ya mashuhuda wamekiri kuwa Bwana Mwasandube amekuwa akijihusisha
sana na suala la ushirikina na kudai kuwa ndiyo silaya yake kijijini
hapo.
Adhabu
hizi kwa watu wanaojihusisha na ushirikina zimekuwa ni nyingi na kali
kwa siku za hivi karibuni, ambapo wengine huchomwa moto na mwingine
kuzikwa akiwa hai mwishoni mwa juma kutokana na kuhisiwa kumuua mpwa
wake kwa imani za kishirikina.
Vitendo
hivi vimelaaniwa vikali na Kiongozi wa Mchifu wa kabila la Kisafwa
Bwana Roketi Mwanshinga, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika
Kata ya Itenzi Jijini Mbeya Aprili 30 mwaka huu ambapo shule tatu za
kata hiyo ziliahirisha masomo ili kupisha tambiko kwa lengo la
kuwafichua wale wote wanaojihusisha na imani za kishirikina kutokana na
kudumaza maendeleo ya wananchi kutokana na kuishi kwa hofu.
Hata
hivyo mara kadhaa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Abbas Kandoro
amewaonya wananchi kutojichukulia sheria mkononi kwani kufanya hivyo ni
kinyume cha sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment