Na Kenneth Ngelesi, Mbeya
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dr Noman Sigalla amelitaka jeshi la polisi kuacha kutumia ubabe na kutopendelea baadhi ya watu wa kada fulani katika kutekeleza majukumu yao kwani kufanya hivyo huchangia watu kutokuwa na imani na jeshi hilo na baadaye kutokea vurugu.
Rai hiyo alitoa na Mkuu huyo mpya wa wilaya mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya wakati akikabidhiwa ofisi hiyo na mtangulizi wake aliyestaafu Evansi Balama ambapo shughuli za makabidhiano zilifanyika siku ya jumatano katika ofisi za Mkuu wa wilaya zilizopo Mbeya mjini.
Dr. Sigalla amesema kuwa kutokana
na uzoefu wake kwamba baadhi ya askari wa jeshi hilo wamekuwa na tabia ya kutoa maamuzi yenye upendeleo wa jamii au vyama fulani hivyo kupekelea vurugu sisizo za lazima.
Amesema kuwa kutokana na wananchi
wengi kuwa na uelewa wa hali juu wamekuwa wepesi wa kung’amua mambo juu
ya utendaji wa baadhi ya askari na wananchi wengi kutokubaliana
na maauzi hayo.
Ametaka wananchi wa wilaya ya
Mbeya kutokuwa tayari kunyanyasika na mtu kutokana na ubaguzi wa
chama, kabila, kwani kwa kufanya hivyo ni kudhorotesha maendeleo ya wilaya na mkoa na taifa pia.
Amesema inapotokea mtu
amevunja sheria za nchi jambo ambalo alisema kuwa hata kuwa tayari
kuona mwanachi yeyote ananyanyasika na jeshi hilo kwa tatizo la
kihitikadi za vyama.
Akizungumzia suala la migororo ya
ardhi alisema kuwa anatambua wazi kuwa ni moja ya changamoto kwake
kwani wilaya aliyotoka ya Hai Mkoani Kilimanjaro ndiko kwenye migogoro
zaidi.
Mkuu huyo wa wa wilaya alisema
hatalifumbia mambo jambo la watumishi wasio waaminifu katika
ofisi yake kwani katika taarifa aliyopata kutoka kwa mtangulizi wake
inaonyesha kuwa watumishi wengi wamekuwa wakitoa taarifa
zisizosahihi hasa wakurugenzi.
Hata hivyo alitoa wito kwa
watumishi wa serikali kufanya kazi kwa kushirikiana na vyombo vya habari
kwani watumishi wengi wamekuwa wakikwepa kufanyakazi na wanahabari.
‘Inasikitisha sana na mara nyingine serikali inalaumiwa na wananchi kwa sababu ya watumishi ambao hawako tayari
kufanyakazi na vyombo vyetu vya habari, sasa unakuta kuna mradi serikali
imetumia zaidi mil 800 lakini siku ya kufungua mnashindwa kuwaita
waandishi wa habari ambao hata malipo yao hayazidi shilingi laki mbili kama mnafanya hivyo mnadhani wananchi watajuaje kwamba serikali yao inafanyakazi’ alisema Dr Sigalla
Kwa upande wake Mkuu aliyemaliza
muda wake wa utumishi Evans Balama alisema wilaya ya Mbeya mjini ni
ngumu kuliko wilaya zote alizowahi kufanyakazi hasa katika utekezaji wa
majukumu ya kiserikali wananchi wengi wamekuwa wabishi.
Aidha amebainisha baadhi ya idara
zenye matatizo na kumtaka Dr Sigalla kuwa makini nazo na zimekuwa
zikileta migogoro mingi ikiwa ni pamoja na Idara ya Ardhi ambayo watumishi wake wengi siyo waaminifu na Jeshi la polisi.
Dr Sigalla ameteuliwa kuwa Mkuu
wa wilaya ya Mbeya hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete akitokea wilaya
ya Hai Mkoani Kilimanjaro uteuzi ulifanyika nchi nzima, na kuapishwa
Mei 16 pamoja na wakuu wote wa wilaya nane za mkoa na Mkuu wa Mkoa huyo Abasi
Kandoro, Ikulu ndogo iliyopo Mbeya mjini na kukabidhiwa jukuma
la kuziongoza halmashauri mbili ambazo ni Mbeya mjini na Mbeya vijijini.
0 comments:
Post a Comment