Klabu ya Bayern imeshinda mechi zake saba za nyumbani mfululizo kuelekea fainali hii dhidi ya Chelsea.
Mara ya mwisho kwa pande hizi mbili kukutana,
ilikua katika robo fainali ya mwaka 2005 ambapo Chelsea ilishinda 6-5
kwa jumla ya mabao ya ugenini na nyumbani.
Wakati huo Petr Cech, John Terry, Ashley Cole, Frank Lampard na Didier Drogba wote walishiriki.
Bayern inataraji kujiunga na Liverpool kama
mojapo ya vilabu vitatu vilivyofanikiwa katika mashindano ya Kombe la
Ulaya ikiwa watashinda kwa mara ya tano.
Klabu iliyopata ushindi zaidi ya Bayern ni Real Madrid na AC Milan.
Bayern imeshinda mara moja na kushindwa mara mbili mara tatu ilipochuana na upinzani kutoka kwa vilabu vya England.
Hii ni mara ya sita katika Kombe la Ulaya kwa
vilabu vya Ujerumani na England kupambana kwenye fainali -na ni mara
moja tu ambapo vilabu kutoka Ligi ya Bundesliga kuibuka na ushindi.
Ushindi wa Bayern utamfanya Jupp Heynckes kua
kocha wa 19 kushinda kombe hili mara mbili, kufuatia ushindi wake wa
1998 alipokua akiifunza Real Madrid.
Ikiwa uwanja wa nyumbani Bayern imeshinda mechi
13 kati ya 14 za michuano ya Ulaya, huku Chelsea ikiwa imeshinda mara
moja tu ikiwa safarini katika michuano ya msimu huu.
Mara pekee ambapo Chelsea ilifikia fainali
ilikua mwaka 2008 mjini Moscow iliposhindwa na Manchester United kupitia
mikwaju ya peneti.
BBC.
0 comments:
Post a Comment