Mbunge
wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mbeya mheshimiwa Dakta Mary Mwanjelwa, akiongea na wananchi wa mwanjelwa katika
kiwanja cha sido, ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika Kongamano
la Maombi la kuuombea Mkoa dhidi ya Vitendo viovu.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa
Mbeya kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dakta Mary Mwanjelwa,
ameshiriki kongamano la maombi dhidi ya kukomesha vitendo viovu Mei 5
mwaka huu.
Kongamano hilo lililoandaliwa na
Kipindi cha Faraja yako kinachurushwa alfajiri na usiku, kupitia Kituo
cha redio cha Bomba FM kilichopo mkoani hapa na kufanyika katika Ukumbi
wa St Mary uliopo Forest Mpya jijini Mbeya.
Kongamano hilo lilifunguliwa na
Askofu wa Kanisa la P.A.G (Pentecost Assemblies of God) Damianus Kongolo
Thomas, likiwa na nia ya kufanya maombi ya kukomesha vitendo viovu
vinavyofanyika mkoani hapa ikiwa ni pamoja na Upigaji ndondo, ushirikina
na ujambazi.
Askofu huyo alimpongeza Mbunge huyo
Dakta Mwanjelwa, kwa kukubali wito licha ya kuwa na majukumu mazito ya
kulitumikia taifa hivyo angeweza kutoa udhuru wowote, lakini pia
alimheshimu Mungu kwa kujumuika na waumini wa madhehebu mbalimbali.
Aidha Mmoja wa watangazaji wa kipindi
hicho Bi Martha Haule alisoma risala na kuelezea umuhimu wa kipindi
hicho ambacho kinagusa jamii mkoani hapa kwa kutembelea wafungwa
gerezani, wagonjwa hospitalini, vituo vya kulelea watoto yatima na
waishio mazingira hatarishi na kutoa wito kwa mgeni rasmi na wananchi
mbalimbali kuwatembelea wahitaji hao kwani ni upendo aliotuachia Bwana
Yesu Kristu.
Akijibu risala hiyo Mgeni rasmi Dakta
Mwanjelwa, amesema ameguswa na huduma nzito inayotolewa na kituo hicho
cha redio kwani wanaigusa moja kwa moja jamii na kusema kuwa wanaisaidia
Serikali na kiasi kikubwa na hii inaonesha jinsi gani watanzania
walivyo na upendo ambapo kwa upande wake anaungana na kipindi hicho
hivyo aorodheshewe vipindi vinavyohitaji msaada.
Hata
hivyo Bomba FM redio hivi karibuni imefanya harambee ya kuchangisha
fedha za ujenzi wa kituo cha kulelea wazee ambapo jumla ya shilingi
milioni 20 zilipatikana kwa njia ya kutoa papo hapo na nyingine kwa
ahadi.
0 comments:
Post a Comment