Kaburi la Nyerere Kombwee (52) (kulia) aliyezikwa akiwa hai, ambapo alifukuliwa na Polisi na baadae mwili wake kuzikwa upya siku ya Jumapili Aprili 29, mwaka huu na kaburi la Mpwa wake Regnand Kombwee ambao wote walizikwa siku hiyo.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Nyerere Kombwee (52) aliyezikwa hai siku ya
Jumamosi Aprili 28 mwaka huu majira ya saa tatu asubuhi amezikwa tena siku ya
Jumapili, siku mojaa baada ya mwili wake kufukuliwa na Jeshi la Polisi saa moja
baada ya kifo chake.
Marehemu huyo alizikwa akiwa hai baada ya
kutuhumiwa kumuua mjomba wake marehemu Regnand Kaombwee, kwa imani za
kishirikina hali iliyowapa hasira nduguze na hivyo kuamua kuchimba kaburi
ambalo ilitakiwa azikwe marehemu aliyefariki kwa ugonjwa lakini badala yake
akazikwa marehemu Nyerere, licha ya kuwasihi wamwachie na angewapa kitita cha
shilingi 200,000.
Hata hivyo nduguze walizikataa na kuendelea kumzika
kikatili huku mara kadhaa marehemu akifanya jitihada za kutaka kujinasua katika
kaburi hilo
kabla hajakandamizwa na chepeo la mchanga ambapo alivuja damu, ambapo
aliendelea kuzilama huku akinuia kwa yeyote aliyemtendea ukatilihuo pindi
akipona basi atakiona kwa maana kwamba atakufa.
Baada ya kifo chake Nyerere Kombwee Polisi walifika
kijijini hapo na kuwatawanya wanaukoo kwa kupiga risasi hewani na kuupeleka
mwili huo katika Hospitali ya Rufaa iliyopo Jijini Mbeya.
Aidha mara baada ya uchunguzi kukamilika Polisi
waliutoa mwili kwa ndugu zake na mazishi ya ndugu hao yalifanyika kwa pamoja
siku ya Jumapili Aprili 29 mwaka huu, kaburi la Marehemu Regnand likiwa kushoto
na kutenganisha ambapo Marehemu Nyerere likiwa na kusimika mti mrefu wa mita
tatu kwenda juu na mita mbili kushuka chini huku mwili wake ukiwa umekandamizwa
sikioni na mti huo aina ya mkaratusi.
Kitendo hicho cha mtu kuzikwa akiwa hai kimelaniwa
vikali na Chifu Roketi Mwanshinga, ambaye amesema hali hiyo isipokemewa watu
watajenga chuki, visasi na mauaji ambayo yanaweza kuepukika na ametoa wito wa
kushirikishwa pindi wanapoona kuwa tetesi ya vitendo vya kishirikina.
0 comments:
Post a Comment