Habari na Rashid Mkwinda, Mbeya.
Jumla ya miradi 9 yenye thamani ya zaidi
ya sh. milioni 291.7 imezinduliwa na kuwekwa mawe ya msingi wakati wa mbio za
Mwenge wa Uhuru uliokimbizwa katika wilaya mpya ya Momba mkoani Mbeya.
Mwenge wa Uhuru ambao umemaliza mbio zake katika
wilaya ya Chunya na kuanza rasmi mbio zake katika wilaya ya Momba na kujenga
historia ya kuwa wilaya ya kwanza mpya kukimbizwa mwenge kati ya wilaya 19 mpya
zilizoanzishwa hivi karibuni.
Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo zimezindua
na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya huduma za kijamii ikiwemo
elimu, Kilimo, afya,Ujasiriamali,Ushirika na hifadhi ya mazingira.
Akitoa taarifa za miradi hiyo mbele ya kiongozi
wa Mbio za Mwenge Kitaifa Kapteni Honest Mwanosa, Kaimu Mkuu wa wilaya ya Momba
Bw. Jofrey Kikosa amesema kuwa kati ya gharama za miradi hiyo jumla ya
sh. milioni 17.2 zimetokana na michango ya wananchi ambapo kiasi cha sh.
milioni 166.6 zimetokana na mchango wa serikali kuu.
Aidha Bw. Kikosa amesema kuwa kati ya fedha hizo
jumla y ash, 342,000 zimetokana na michango ya wahisani ambapo kiasi cha
sh. zaidi ya sh milioni 91 ni michangi ya watu binafsi huku kiasi cha zaidi ya
sh milioni 7 zimetokana na mchango wa halmashauri ya wilaya.
Kwa upandee wake Ofisa Utumishi wa wilaya ya
Mbozi Bw. Noeli Abel ambaye amesoma risala ya Mbio za Mwenge kwa niaba ya
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo alisema kuwa miradi iliyofunguliwa na
bio za wenge wa Uhuru ni pamoja na mradi wa Biogas uliopo katika kijiji cha
Chole,Ujenzi wa zahanati na ujenzi wa hosteli ya wasichana shule za sekondari
Ivuna na Chitete.
Ameitaja miradi mingine kuwa ni pamoja na
ujenzi wa nyumba ya kulala wageni iliyopo kijiji cha Ntungwa,
kukagua mradi wa nyuki,ujenzi wa shule ya chekechea Parokia ya Chitete na
ujenzi wa nyumba ya mratibu wa elimu Chitete.
Akizungumzia ujumbe wa mwenge wa Uhuru mwaka
2012,kiongozi wa mbio za mwenge Kapt.Mwakanosa amesema kuwa mbio za mwenge
mwaka huu zimelenga katika hamasa ya kujitokeza katika sensa ya watu na
makazi Agosti 26 ambayo ni wajibu wa kila mwananchi kujitokeza kuhesabiwa kwa
nia ya kuirahisishia serikali mipango yake ya maendeleo kwa watu wake.
Pia Kapteni mwanosa amewataka wananchi
kujitokeza kutoa maoni juu ya marekebisho ya Katiba ambayo yataliwekea Taifa
mkataba na wananchi wake na serikali kwa nia ya kuboresha mahitaji muhimu
ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.
0 comments:
Post a Comment