Pages


Home » » NDUGU WA USUSIA MWILI WA MAREHEMU KWA SIKU MBILI, KUTOWATEMBELEA NDUGUZE NDO CHANZO MASKINI MAUMIVU YA NONDO YAMSABABISHIA KIFO.

NDUGU WA USUSIA MWILI WA MAREHEMU KWA SIKU MBILI, KUTOWATEMBELEA NDUGUZE NDO CHANZO MASKINI MAUMIVU YA NONDO YAMSABABISHIA KIFO.

Kamanga na Matukio | 05:16 | 0 comments
*Wadai marehenu hakuwajali.
*Mwili washinda ndani ndugu watokomea.
*Balozi wa mtaa aokoa jahazi.
******
Habari kamili na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Familia ya Edson Mbembela wa Nzovwe imejikuta ikiingia matatani baada ya kuutelekeza mwili wa ndugu yao aliyekuwa mjane ambaye aliolewa na mwanawe Ebnesa Mbembela aliyefariki mwaka 2005.

Marehemu alikuwa akiishi mtaa wa Iyela jijini Mbeya na kufariki Mei 7 mwaka huu majira ya saa nene mchana katika nyumba inayomilikiwa na Bwana Giseon Kyebeleka, ambaye ni Askari magereza wa Chuo cha Magereza Kiwira mkoani Mbeya.

Aidha inadaiwa marehemu alifariki kutokana na maumivu ya kichwa kutokana na kupiga nondo hivi eneo la Sido jijini hapa alipokuwa anarejea nyumbani majira ya usiku.

Balozi wa Mtaa huo Bwana Lwitiko Mwanyingili amesema marehemu alijaaliwa kupata watoto wanne, ambapo wawili walikuwa wakiishi na marehemu kabla ya kifo chake na mara baada ya kufariki walimtafuta baba mkwe Bwana Edson Mbembela na kumtaarifu juu ya kifo cha mkwewe.

Baada ya taarifa hizo Bwana Mbembela na mkewe Bi Maria Mbembela (70) walidai hawako tayari kuzika kwa vile marehemu hakumuuguza marehemu mmewe aliyefariki mwaka 2005 na pia alikuwa hawatembelei nyumbani.

Aidha Baba mkwe huyo aliagiza ndugu wa marehemu huyo wamzike na baada ya mazishi aletewe watoto hao kwa ajili ya kuwatunza.

Uapnde wa pili wa ndugu wa marehemu nao walikataa kumzika wakidai kuwa binti yao walimuoza kwa ukoo wa Mbembela na pia marehemu alikuwa hawatembelei hivyo hawana haki ya kumzika.

Balozi Mwanyingili aliamua kumtaarifu Mwenyekiti wa mtaa wa Iyela Bwana Japhet Mwangonele ambapo alizikutanisha pande zote mbili bila mafanikio na hata alipotoa taarifa Kituo cha Polisi Mwanjelwa nao hawakuwa nala kufanya.

Naye, Mchungaji wa Kanisa la Church of God Solomon Mwashoma, amesema amesikitishwa sana na tukio hilo na kumhukumu marehemu kwani huo ni ukatili.

Mchungaji huyo ameenda mbali sana kwa kusema si vema kuwanyanyasa wajane na hii ni hatari zaidi kwa jamii ya kitanzania na kuwaasa watu wenye tabia kama hizo kuacha mara moja.

Pia viongozi mbalimbali wa mtaa wameaswa kutowapokea watu bila kuwa na barua za mahali walikotoka kwani iliwachukua muda ilikuzipata koo zote mbili kutokana na marehemu kuhamia mtaani hapo wiki mbili zilizopita.

Hata hivyo baada ya kushindwa kupatikana kwa muafaka balozi huyo wa mtaa Bwana Mwanyingili alitoa shilingi 25,000 kwa ajili ya kuupeleka mwili wa marehemu Hospitali ya rufaa Mbeya kusubiri maafikiano ya ndugu wa pande zote mbili waishio Nzovwe.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger