Pages


Home » » Mtu mmoja amefariki dunia Mkoani Mbeya baada ya kutokea kwa ajali ya barabarani,

Mtu mmoja amefariki dunia Mkoani Mbeya baada ya kutokea kwa ajali ya barabarani,

Kamanga na Matukio | 05:20 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mtu mmoja amefariki dunia Mkoani Mbeya baada ya  kutokea kwa ajali ya barabarani, Mei 16 mwaka huu, majira ya saa 1 kamili jioni eneo la Mpemba Tunduma, Wilaya mpya ya Momba Mkoani Mbeya.

Gari lenye nambari T 758 BBV aina ya RAV 4 lililokuwa likiendeshwa na dereva aitwaye Joseph Daudi (30) mkazi wa Ileje lilimgonga mtembea kwa miguu Elisha Sikana (13) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mpemba na kusababisha kifo chake papo hapo.

Dereva huyo amekamatwa na gari lake lipo kituo cha Polisi cha Tunduma na chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi.

Hata hivyo Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba upelelezi wa tukio hili unaendelea.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger