Mmoja
wa wananchi waliojeruhiwa kwa kipigo kufuatia mapigano yaliyozuka
katika Kijiji cha Chilulumo Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya Bwana Daudi
Sikali.
Mabinti
waliodhalirishwa kijinsia baada ya kubakwa na watu saba walionadaiwa
kushinikizwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Chilulumo, Wilaya ya Mbozi,
Mkoani Mbeya Bwana Bruno Chipungu, huku wakishikiwa mashoka kutenda
ukatili huo wa ubakaji kwa mabinti. (Picha na Maktaba yetu)
*******
Makala na Ester Macha, Mbeya.
Pamoja na serikali na asasi zisizokuwa za kiserikali kuendelea kupinga
vitendo vya kikatili kwa wanawake lakini hali hiyo imeendelea kufanyika katika
jamii kwa wabinti kufanyiwa vitendo vya kikatili na kidhalilishaji pasipo
kuogopa mkondo wa sheria.
Vitendo hivyo kwa siku za karibuni vilianza kupungua kutokana na serikali
kuingilia kati na vyombo vya dola na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali lakini
hali hiyo imeonekana kuanza kurudi kimnya kimnya tena cha kushangaza viongfozi
wa serikali za vijiji ndo wamekuwa wakishiriki katika unyama huo.
Kutokana na hali hiyo hivi karibuni wasichana wawili wa familia moja wamefanyiwa
ukatili wa kinyama baada ya kubakwa kwa zamu hadi kupoteza fahamu na kundi la
vijana waliovamia nyumbani kwao.
Katika tukio hili la kusikitisha kwa wasichana hawa limeonekana kufanywa na
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chilulumo kwa kutumia vijana sita ambapo mwenyekiti huyo alikuwa akitoa amri kwa
vijana hao kufanya unyama huo tena kwa kujiamini .
Kinachoonekana kuuma kwa tukio hili la wasichana kwa jinsi kiongozi huyu
alivyoweza kutumia madaraka yake kufanya ukatili huo huku akisahau madfaraka
aliyopewa na serikali.
Viongozi wa serikali kama hawa tunajua wao ndio wa kwanza kukemea matukio
haya lakini cha ajabu kiongozi huyu amegeuka kuwa samba badala ya kukemea tabia
ya ubakaji inayofanywa katika jamii.
Katika hali ya kawaida kiongozi huyu hakustahili kufanya kitendo hiki cha
kinyama na kama alikuwa analipiza kisasi kwa wazazi wa watoto hao hakustahili
kufanya hivyo kwani inaonyesha ni jinsi gani kiongozi huyu asivyofuata maadili
ya kazi yake na inaonekana kuwa amekuwa
akifanya vitendo hivyo kwa kutumia cheo chake isipokuwa ilikuwa haijagundulika.
Tukio hili limeonekana kuvuta hisia za wakazi wa Mkoa Mbeya na Wilaya ya
Mbozi kwa kumlalamikia mwenyekiti huyu wa kijiji kufanya ukatili huo wa ajabu
kwa wasichana hao wadogo ambao ni taifa la kesho.
Ninachoamini hapo ni kwamba Mwenyekiti huyo wa kijiji inaonyesha kuwa
alikuwa analipa kisasi ambacho anajua yeye kwani kwa hali ya kawaida kwa
wabinti wadogo kama hawa sidhani kama kuna jambo kati ya wasichana hawa na mwenyekiti huyu kwa upeo
wangu na akili yangu nafikiri kuwa ni
kulipa visasi kutokana na mwenyekitri huyo kuwa na tofauti na wazazi wa wasicchana
hao.
Bila aibu Mwenyekiti huyu aliamurisha
vijana hao kuvunja nyumba hiyo majira ya saa 3 usiku akiwa na vijana na kuumuru
kuwafunga midomo wasichana hao kwa kutumia shuka ambazo walikuwa wamejifunika
ili wasiweze kupiga kelele.
Ni kweli azima yao ilitimia huku Mwewnyekiti huyo wa Kijiji akiwa amesimama
pembeni wakati vijana hao wakiendelea kuwabaka wasichana hao kwa zamu mpaka
pale walipopoteza fahamu kutokana vijana hao kuwa wengi.
Ninachojiuliza ni kwamba mwenyekiti huyu alipata wapi ujasili huu wa
kufanya kitendo hicho cha kinyama na kama alikuwa akosana na moja ya familia ya
wazazi wa watoto hao kwanini amuue kulipiza kisasi kwa watoto hao?.
Wasichana hawa wa familia moja wamewfanyiwa unyama ambao hawawezi kusahau
katika maisha yao kwani hilo ni kovu ambalo haliwezi kufutika maishani mwao
kwanza ndani ya akili yao tayari wameharibika kisaklojia .
Kwa tukio hili ambalo wamefanyiwa wasichana hawa kuna hatari ya kuwa wameambukiz
ugonjwa wa ukimwi na magonjwa mengine ya
ngono. Ni wajibu wa Hospitali ya Wilaya ya Vwawa kuhakikisha wasichana hawa
wanachukuliwa vipimo vyote ili kujua
kama wameathirika au wazima .
Ninachoshauri ni kwamba vyombo vya dola vihakikishe Mwenyekiti huyu
anachukuliwa hatua kali za kisheria kwa unyama huu aliofanya hasa ukizingatia
kuwa yeye ni kiongozi wa serikali ambaye anatakiwa kuwa mfano lakini bado aliamua kufanya kitendo hicho
bila aibu.
Tukio hili limefanyika marchi 11 mwaka
huu majira ya saa 3 usiku wakati wasichana hao ndugu wakiwa wamela
chumbani kwao na kufanyiwa ukatili huu
uliomshirikisha Mwenyekiti huyu wa Kijiji .
Nionavyo mimi mashirika ya kutetea haki za binadamu yaingilie kati
suala
hili mpaka kujua mwi
sho wake kwani natambua kuwa mwenyekiti huyu
hajakamatwa kutokana na tamaa zilizojengeka kwenye vyombo vya dola bila
ya kuwa na huruma na watu wanaofanyiwa unyama huu.
Kwa uzito wa tukio hili jeshi la polisi halina budu kuweka tamaa pembeni kwa
kuhakikisha kuwa mwenyekiti huyu anachukuliwa hatua pamoja na vijana sita
walioshiriki kufanya unyama huo.
Sawa Mwenyekiti huyu tayari yupo kwenye mikono ya sheria je lakini
ninachokiona hapa ni ni kwamba wanasubiri waliopatwa na kitendo hicho wasahau kasha
tukio hilo linaendelea kupigwa kalenda tu kuwa ushahidi bado.
Ushahidi upi ambao unatafutwa na jeshi la polisi wakati walengwa hao walimwona mwenyekiti wa
kijiji hicho baada ya kuvunjwa mlango wa chumbani akiwa na vijana sita sasa
kipi kitakuwa kinakwamisha wakati suala hilo
linajieleza.
Hata hivyo wasichana hao wakieleza kwa uchungu wakiwa katika hospitali ya
Vwawa walisema kuwa walipoingia ndani, walimwona mwenyekiti wa
kijiji hicho, akiwaamuru vijana hao kuwafunga macho kwa kutumia shuka
waliyokuwa wamejifunika na kisha wakaanza kubakwa kwa zamu.
Mmoja wa wasichana hao aliyebakwa alisema yeye alibakwa na watu wawili na kupteza fahamu fahamu, baada ya hapo
sikujua kilichoendelea mpaka nilipozinduka alfajiri nikajihisi nina maumivu
makali sana nadhani waliendelea kunibaka hata nikiwa sina fahamu na
nilipozinduka nikamwona mwenzangu akiwa na hali mbaya zaidi.
Msichana mwingine alisema kuwa alibakwa na vijana wengi ambao walikuwa
wakiamrishwa na mwenyekiti wa kijiji, baada ya kuwafunga usoni kwa kutumia
mashuka yao ambayo walikuwa wamejifunika huku mwenyekiti huyo akiwakataza kupiga kelele kwa vitisho vya kuwaua.
Lakini cha kushangaza tena Ofisa Mtendaji wa kata ya Chilulumo alikataa
kutoa barua kwa wasichana hao kwa madai muda wa kazi umeisha, hii inaonyesha ni
jinsi gani viongozi hao wasivyojali
matatizo ya wananchi wao hata ile huruma ya kuwaona wasichanma hao wakilia kwa
uchungu lakini bado mtendaji huyo aliendelea kufunga ofisi yake.
Hata baada ya kufika hospitali Wasichana hao hawakupata huduma yoyote zaidi
ya kupewa vidonge vya homa na kutakiwa kurudi nyumbani, huku wakisikia maumivu
makali sehemu zao za siri.
Walisema siku iliyofuata walifika askari polisi wakiongozana na Mkuu wa
Wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimoro na kuwahoji lakini hawakumkamata mwenyekiti wa
kijiji hicho, licha ya kuwahakikishia kuwa alishiriki katika uhalifu huo.
Wasichana hao walisema kuwa pamoja na viongozi hao kuwaona wakiwa katika
hali mbaya hawakuwapatia msaada wowote wa kuwapeleka hospitali.
Lakini pia kinachoonekana kushangaza ni kwamba pamoja na Mwenyekiti wa
kijiji hicho na Ofisa Mtendaji kuonekana kushiriki katika tukiuo hilo lakini
bado hawakuweza kukamatwa na jeshi la polisi kwa madai hawafahamu kitu kama
hicho na badala yake walikamatwa watu wengine tu wakati wahusika wakuu wapo.
Hili jeshi letu linawekwenda wapi ,wasichana hao wamesema ukweli kuwa
walioshiriki katika tukio hilo ni mwenyekiti na Mtendaji iweje washindwe
kukamatwa wakati ushahidi upo?.
Nakuomba Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya wachukulie hatua mwenyekiti na Mtendaji kuwa na uchungu kama
hao ni watoto wako kwanini ushindwe
kuamini maneno ya wasichana hao unatafuta ushahidi upi ?.
Lini jeshi la polisi litabaini kuwa walishiriki wakati walengwa tayari
wamesema hao ndo walioshiriki ukweli upi unatafutwa ili polisi waweze
kuamini ?kwa kufanya hivyo unasababisha matukio hayo
yazidi kuendelea katika kata hiyo, na hata kama siyo hapo inaweza
kutokea
sehemu nyingine tofauti na hapo ifike wakati jeshi la polisi lifanye
kazi yake
kwa uaminifu na si kuumiza wanannchi .
0 comments:
Post a Comment