Pages


Home » » MKE WA SITA WA MFALME MSWATI AONDOKA NYUMBANI, ADAI KUDHARIRISHWA KIJINSIA.

MKE WA SITA WA MFALME MSWATI AONDOKA NYUMBANI, ADAI KUDHARIRISHWA KIJINSIA.

Kamanga na Matukio | 05:14 | 0 comments
Mke wa sita wa mfalme mswati wa tatu Swaziland ameondoka na kuyaacha makazi ya kifalme alikokua akiishi, Baada ya kuishi kwa miaka mingi na mume wake, Angela Dlamini ameondoka baada ya kuteswa, kunyanyaswa na kudhalilishwa kijinsia na mumewe.
Inaaminika Angela ameishi bila furaha kwa muda mrefu na alitaka kuondoka kwenye makazi ya mumewe miaka kadhaa iliyopita, na sasa amekua mwanamke wa tatu kuondoka kwenye makazi ya mfalme huyo.
Mke wa kwanza wa king Muswati kuondoka kwenye makazi ya kifalme alikua Delisa Magwaza mwenye umri wa miaka 30 ambae aliondoka kwenda London na watoto wake watatu, Aliefata ni Putsoana Hwala mwenye umri wa miaka 30 pia ambae aliondoka na watoto wake pia.
Kwenye sentensi nyingine ni kwamba Mke wa 12 wa muswati Nothando Dube mwenye umri wa miaka 22, alipewa na mumewe kifungo cha ndani ya nyumba baada ya kugundulika kwamba alikua na uhusiano wa kimapenzi na waziri mmoja wa Swaziland ambae nae alifukuzwa kazi pia ambapo Mwanamke huyo bado yuko na Muswati na inasemekana anavumilia mateso kwa sababu tu hawezi kuwaacha watoto wake.
Mwezi uliopita katika birthday yake ya 44 mfalme huyo mwenye wake 13, alizawadiwa JET japokua nchi hiyo iko kwenye hali mbaya kiuchumi huku Waziri mkuu akithibitisha kwamba mfalme huyo sasa hivi anamiliki McDonnell Douglas DC-9 twin-engine Jet.
Kwa hisani ya millardayo.com
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger