Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho
Bwana David Mwankina (kushoto), akifuatiwa na Askofu wa Kanisa la
Moravian Tanzania Alinikisa Cheyo, Mgeni rasmi Dr Victoria Kanama na
Mkuu wa Chuo hicho cha Ualimu Eliackim Mtawa.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Askofu kiongozi wa Kanisa la Moravian Tanzania Alinikisa Cheyo, amewataka waumini kuthamini elimu ili kuleta tija katika jamii.
Ameyasema
hayo alipokuwa akifungua maombi kwenye Chuo cha Ualimu cha Kanisa la
Moravian Mbeya katika mahafali ya pili ya chuo hicho Mei 3 mwaka huu
jijini Mbeya.
Akinukuu
baadhi ya vifungu katika biblia Askofu Cheyo amesema wazazi na walezi
wanapaswa kuwajengea msingi wa elimu vijana kwani ndio urithi utakao
wasaidia maishani mwao, badala ya mali kwani mali huisha au kupotea.
Kwa upande wake mgeni rasmi Dr
Victoria Kanama, ambaye ni Mkurugenzi wa Hospitali ya K'S iliyopo jijini
hapa na pia ni Mkuu wa Bodi ya Chuo Kikuu cha TEKU, amewataka wahitimu
kufuata maadili mazuri ya ualimu na hivyo kuwa mabalozi wazuri wa chuo
hicho, ambapo pia alikazia suala la kujiendeleza kielimu zaidi na
kutobweteka.
0 comments:
Post a Comment