Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Watu wawili wamefariki dunia, katika matukio mawili ya ajali ya barabarani wilayani Mbarali na Rungwe, Mkoani Mbeya.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani
hapa Advocate Nyombi amesema ajali ya kwanza iliyotokea katika Wilaya ya
Mbarali, mei 20 mwaka huu majira ya saa 10 jioni barabara ya
Mbeya/Iringa gari nambari T 536 APU likiwa na tela lenye nambari T 330
APD aina ya Scania.
Gari hilo lilikuwa likitokea Jijini
Dar es salaam kuelekea mkoani Mbeya likiendeshwa na dereva aitwaye
Ismail Kiteve iliacha njia na kupinduka kisha kusababisha kifo chake.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika
Hospitali ya Wilaya hiyo iliyopo Rujewa, na chanzo cha ajali hiyo
kimetajwa kuwa ni mwendokasi na upelelezi wa tukio hili unaendelea.
Aidha, Kamanda Nyombi amesema ajali
nyingine imetokea Wilaya ya Rungwe majira ya saa 7 mchana, eneo la
Katela barabara ya Mbeya/Tukuyu wilayani humo ikihusisha gari aina ya
Toyota Coaster lenye nambari T 672 AWK.
Gari hilo lilikuwa likiendeshwa na
dereva aitwaye Steven Mwambola(40), mkazi wa Mtaa wa Bagamoyo Tukuyu
ilimgonga mwendesha pikipiki nambari T 628 BUL aina ya T-Better aitwaye
Salim Jimu(26), mkazi wa Ntokela na kusababisha kifo chake papo hapo na
abiria wake Gody Julius(17) kujeruhiwa.
Hata hivyo majeruhi huyo amelazwa
katika Hospitali ya Mission Igogwe na dereva wa gari amekamatwa na gari
lipo kituo cha polisi, kutokana na mwendokasi uliyopelekea ajali hiyo
na upelelezi wa tukio hili unaendelea.
0 comments:
Post a Comment