Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Watu 6 wa familia moja wamenusurika
kifo baada ya moto kuzuka katika mtaa wa Ilolo, Kata ya Ruanda, Jijini
Mbeya, Mei 17 mwaka huu.
Tukio hilo limetokea baada ya familia
hiyo ya Bwana Ezekiel Mwasandube na mkewe Bi Christina Kyamba kulala na
moto huo kuanzia sebuleni, ambapo inadaiwa kuwa dirisha la nyumba yao
lilivunjwa na mtu au watu wasiofahamika kisha kuwasha moto kwa kutumia
ufagio wa kupigia deki(mopu) ulionyunyiziwa mafuta ya taa na baadae
kutokomea kusikojulikana.
Wengine walionusurika ni pamoja na
Eva Mwasandube ambaye mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari
Sinde na Tabea Mwasandube ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha sita katika
shule ya Sekondari Meta na William Mwasandube.
Wazazi walisikia yowe kutoka kwa
watoto wao Eva na Tadea na walipojaribu kutoka kujua kulikoni ndipo
wazazi walikumbana na wingu nzito la moshi ndipo waliomba msaada kwa
majirani ambao walifika na kuvunja mlango na madirisha yaliyokuwa na
vizuizi (grill) na kuwaokoa wanafamilia hao.
Baada ya tikio hilo Bi Kyamba na
wanawe Eva na Tadea walizirai na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa
iliyopo Jijini Mbeya na hali zao zinaendelea vema.
Naye, Balozi wa mtaa Bwana Joseph
Mwambapa na Mwenyekiti wa mtaa Benson Mbwana walifika haraka na kuwaomba
wakazi wa eneo hilokusaidia kuzima moto.
Hata hivyo Kamanda wa Jeshi la Polisi
mkoani hapa Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kwamba Jeshi lake wanafanya uchunguzi kuhusiana na tukio hili.
0 comments:
Post a Comment