Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mwenyekiti
wa Kitongoji cha Ilembo "A", Kata ya Vwawa, Wilaya ya Mbozi Mkoani
Mbeya Bwana Raphael Kibona, anatuhumiwa kuuza mbuga inayomilikiwa na
mtaa huo kwa watu binafsi zaidi ya 30 na kufanya makazi ya kuishi
tofauti na makusudio ya Kijiji na Serikali kwa ujumla.
Hifadhi
hiyo ambayo hutoa chemichemi ya maji kwa Mto Mkusi Nkana na Mto Momba
ipo hatariki kukauka kutokana na Mwenyekiti huyo kuendelea kuuza viwanja
hivyo vya mbuga na pesa zote kujimilikisha licha ya malalamiko ya
wananchi wa mtaa huo kumtaka kuacha mara moja.
Katika
mkutano uliofanyika Mei 7 mwaka huu kijijini hapo, Mzee wa Kimila Bwana
Witson Mwampashi, aliangua kilio kutokana na Bwana Kibona kutowaheshimu
viongozi wa kimila na wananchi wa mtaa huo kwani muda wote waliitunza
hifadhi hiyo ili iwe manufaa kwa vizazi na vizazi.
Aidha
alipotaka kujieleza katika mkutano huo ni kwanini ameuza maeneo hayo ya
mbuga mwenyekiti huyo alijibu kwa kujiamini kuwa ameshtukizwa swali hilo
hivyo hayupo tayari kujibu tuhuma hiyo hali iliyofanya wananchi
kutaharuki kabla ya kutumika busara za Mwenyekiti wa mkutano huo Bwana
Henry Singogo ambaye aliwataka wananchi kuwa watulivu ili watoe maamuzi
ambayo yatasaidia mtaa huo kuokoa hifadhi hiyo.
Mara
Kadhaa mtuhumiwa huyo aliitwa kwenye vikao vya mtaa na mara mbili kukiri
kufanya makosa ya kuuza viwanja hivyo na kujimilikisha pesa mwenyewe na
kuomba asamehewe.
Mkutano
huo ulichrfuriwa na kauli ya Katibu tarafa wa Vwawa Bi Kasunga
alipotumwa na Mkuu wa wilaya ili kutatua mgogoro huo na kuwa kauli yake
ya kuwataka wananchi wapige kura kwamba Bwana Kibona asamehewe au la na
baadhi kudai asamehewe.
Kutokana
na kauli hiyo ya Katibu tawala wananchi hao walisema kuwa tangu lini
mwizi akapigiwa kura pindi anapokiri kuiba, hivyo wametaka mtuhumiwa
huyo akamatwe kwa kujipatia fedha kinyume cha sheria na hivyo uhujumu wa
kiuchumi.
Mtendaji
wa Kitongoji hicho cha Ilembo ameuambia mkutano huo kwamba yeye
anajitahidi kuzuia eneo hilo lisiendelee kuuzwa lakini amekuwa
akizungukwa na mwenyekiti huyo hivyo kuleta kero.
Kwa
uchungu wananchi hao wamemtaka Afisa mtendaji kuorodhesha wale wote
waliouziwa viwanja na gharama zake walizotoa ili pesa hizo ziwakilishwe
kwenye mtaa huo na zisaidie ujenzi wa shule kijijini hapo ambazo ni
shule ya Ilembo na Mtumbo ambazo zinaraslimali lakini hazina maendeleo
yoyote licha ya kuwepo mji, hali baadhi ya wachache kujinufaisha.
Mkutano huo ulifungwa bila kuwa na muafaka na Mwenyekiti kukimbilia Godown kwa hofu ya kipigo.
0 comments:
Post a Comment