Bwana Oscar
Mbalamwezi (47) mkazi wa mtaa wa Chemchemi Kata ya Igawilo jijini
Mbeya aliyepigwa nondo majira ya saa saba usiku wakati akitoka
kuangalia mpira jana, akiwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa iliyopo
jijini hapa.(Picha na maktaba ya mtandao huu)
******
Habari na Yohana Katema, Mbeya.
Wakazi wa Kata ya Iyela Jijini Mbeya
wameulalamikia uongozi wa Serikali ya mtaa, halmashauri na jeshi la
polisi kushindwa kudhibiti vitendo vya upigaji nondo pamoja na kuboresha
miundombinu ya elimu na barabara.
Baadhi ya wakazi wa kata hiyo
Lusekelo Mwalukasa, Ipyana Malangalila na Yusuph Mwakafilwa wamesema
mara kwa mara wamekuwa wakitoa malalamiko ya ujenzi wa barabara, vyumba
vya madarasa vya shule ya sekondari ya kata pasipo mafanikio ya aina
yoyote.
Aidha wamesema licha ya zaidi ya watu
6 kupingwa nondo katika kipindi kifupi hakuna jitihada zozote ambazo
wameziona zikichukuliwa na uongozi wa kata katika kuwapata wahusika wa
natukio hayo.
Kwa
upande wake Afisa mtendaji wa Kata hiyo Ezekiel Kipako, amesema suala
la uboreshaji wa barabara linaendelea, ambapo barabara yenye urefu wa
kilometa moja na nusu itajengwa kwa kiwango cha lami na suala la upigaji
nondo upelelezi unaendelea ili kuwabaini wahusika wa watukio hayo.
0 comments:
Post a Comment