*Watafuna maelfu ya pesa za kijiji,
*Ng'ombe aliyetolewa kama zawadi auzwa,
*Mabati ya msaada yachakachuliwa,
*Wakusanya pesa bila stakabadhi.
*******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Nsonyanga, Wilaya Mbarali, Mkoani Mbeya Bwana Asumile
Mtawa, anatuhumiwa kwa kufuja pesa za kijiji hicho kwa kushirikiana na
wajumbe wa halmashauri ya kijiji na kushindwa kutoa taarifa za mapato na
matumizi kwa zaidi ya miezi mitano.
Wengine
wanaotuhumiwa katika sakata hilo ni Bwana Zacharia Mdolo(mtunza
hazina), Kaisi Jonathan(M/kiti wa Kitongoji cha Nsonyanga), Anjela
John(mjumbe), George Benard Mwambogo (M/kiti wa Kitongoji cha Mkoji), na
Alimwene Saidi(mjumbe).
Lakini
Asunile Mtawa na Kaisi Jonathan wanatuhumiwa kwa kuuza ng'ombe wa
kijiji aliyetolewa na mwekezaji kijijini hapo Desemba 5, 2011 kwa ajili
ya kufanya sherehe na lakini badala ya kufanya sherehe viongozi hao
walimuuza na fedha hazikuwakilishwa katika mfuko wa kijiji.
Aidha
Mtunza hazina wa kijiji hicho Bwana Mdolo, ambaye alipewa dhamana ya
kutunza mabati 20, yaliyotolewa na mbunge mstaafu kwa ajili ya kujengea
ofisi ya kijiji yeye kwa makusudi aliyatumia mabati 13 kwa matumizi
binafsi na kubakia mabati 7.
Baada
ya kubanwa na wananchi hao alifanikiwa kuyarejesha mabati 13 ya gauge
30, badala ya gauge 28 ya awali kinyume na ubora ambao umeidhinishwa na
serikali kwani bati hizo zilinunuliwa mitaani na si katika bohari ya
serikali.
Wakionesha
kukasirishwa zaidi na ufujaji huo wa mali za kijiji wananchi hao,
wamebaini kuwepo kwa uchakachuaji wa pesa za kijiji hicho mathalani
kijiji kililipwa jumla ya shilingi 1,500,000 na mwekezaji lakini
waliwasilisha shilingi 1,450,000, shilingi 800,000 zilikuswa kwa ajili
ya mradi wa maji na zilipotakiwa ziliwasilishwa shilingi 300,000.
Aidha
mchango kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu zilikusanywa shilingi
1,697,500 lakini ziliwasilishwa shilingi 1,060,000 pia shilingi 320,000
zilikusanywa kwa ajili ya mtaa wa Mkoji hazikuoneshwa kabisa.
Pia
viongozi hao walikusanya shilingi 300,000 kwa ajili ya ukarabati wa
Ofisi wa serikali ya kijiji lakini zilitumika shilingi 230,000.
Hawakuishia
hapo viongozi hao walihujumu mbao zilizotolewa na mwekezaji kwa ajili
ya ukarabati, na mbao 6 hazijulikani zilipo zenye thamani ya shilingi
36,000, mfuko wa saruji haifahamiki ulipo baada ya viongozi hao kupokea
mifuko 10, wakahodhi lakini mifuko ilipodaiwa na wananchi ilikabidhiwa
mifuko 9 tu ikidaiwa mfuko huo uliuzwa kwa ajili ya pesa za kumlipa
fundi seremala.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mhongole Bwana Jandika Kisinza,
amesema amesikitishwa sana na kitendo kilichofanywa na viongozi hao
kwani wamekiuka kabisa maadili ya uongozi na kwamba ni kinyume kabisa
cha sera za Chama Cha Mapinduzi, hivyo amewataka kurejesha mara moja
mali hizo.
Mkutano
huo ulisimamiwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nsonyanga B, Bwana June
Rasmus, Afisa Mtendaji wa Kijiji Medson Kilemile, Katibu mipango na
fedha Mengo Rais, Erica Rams Mbogela, Daimon Njelwa, Juma Afrika
Mwambopo(wote ni wajumbe) na Greyson Mololo, Anania Gervas, John
Mwansaso, Ayoub Kabila na Martin Daud.
Mkutano
huo ulianza kwa kupeleka muhtasari wa kikao kwa Mkurugenzi(w), Mbarali
ili kupata muongozo wa hatua za kuchukua kwa viongozi waliohujumu Kijiji
cha Nsonyanga.
0 comments:
Post a Comment