Mbunge
wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mbeya mheshimiwa Dakta Mary Mwanjelwa mbunge
wa viti maalum mkoa wa mbeya akiongea na wananchi wa mwanjelwa katika
kiwanja cha sido, ambaye anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika Kongamano
la Maombi la kuuombea Mkoa dhidi ya Vitendo viovu.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Kongamano la Maombi ya
kuuombea Mkoa wa Mbeya, dhidi ya vitendo viovu vikiwemo vya upigaji
nondo, kujichukulia sheria mkononi, uchunaji ngozi, mauaji ya albino,
watoto na imani za kishirikina litafanyika leo katika Ukumbi wa Shule ya
Sekondari St Mary iliyopo Forest mpya jijini Mbeya.
Mgeni rasmi katika
Kongamano hilo anatarajiwa kuwa Mbunge wa viti Maalumu wa Mkoa wa Mbeya
Dakta Mary Mwanjelwa, ambapo atafuatana na viongozi mbalimbali wa
Serikali mkoani hapa.
Kongamano hilo
limeratibiwa na Kipindi cha Faraja yako kinachorushwa kila siku kuanzia
saa 11:00 alifajiri mpaka 12:30 asubuhi na saa 3:00 usiku mpaka 4:00
usiku katika kituo cha Kurushia matangazo cha Bomba FM redio, kupitia
masafa ya 104.0 kilichopo mkoani hapa.
Aidha, baadhi ya vitendo
vilivyotokea hivi karibuni mkoani hapa ni pamoja na kupingwa nondo
Muimbaji wa nyimbo za Injili nchini Bwana Medrick Sanga, Aprili 10 mwaka
huu wakati akienda katika studio za kurekodi muziki maarufu kwa jina la
Mbeya Records iliyopo ndani ya Kanisa la KKKT Usharika wa Forest.
Hata
hivyo mbali na tukio hilo watu kadhaa wamedaiwa kuuawa kwa imani za
kishirikina na mwingina kuzikwa hai baada ya kuhusishwa kuwa ni mchawi
na pia watoto wa shule kuanguka mara kwa mara wawapo mashuleni kwao.
0 comments:
Post a Comment