Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mzimu
wa viongozi wa Mitaa na Vijiji kukihama Chama cha Mapinduzi (CCM) na
kuhamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), umezidi kushika
kasi baada ya viongozi wawili wa ngazi ya juu katika Kata ya Ilembo
Wilaya ya Mbeya Vijijini, kukihama chama hicho tawala huku wakiongozana
na wenzao sita Mei mosi mwaka huu.
Viongozi
hao waliohama ni pamoja na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Moravian, Kijiji
cha Shizuvi, Kata ya Ilembo Bwana Jongile Anosisye na Katibu wa CCM
tawi la Shizuvi Bwana Yisambi Patikala, ambao wamesema wao kama viongozi
wamechoshwa na kauli ya chama tawala ambazo hazitekelezwi.
Mathalani
wameongeza kuwa waliahidiwa kupewa Kata kwa kipindi cha miezi sita tu,
ukosefu wa barabara ya kutoka Ilembo hadi Shizuvi kwa muda mrefu.
Viongozi
hao waliambatana na wanachama wengine 6 kuhamia CHADEMA ambapo ni
pamoja na Bakulege Kwandende, George Tamali, Binoni Andambike, George
Msabilwa, Mwakalebela Mwasenga na Raphael Mwasenga.
Aidha
viongozi hao pamoja na wanachama walipokelewa na Katibu Kata wa chama
hicho walichohamia Bwana Semi Mawingo na Katibu mwenezi Christopher
Mwambamba na Mwenyekiti Bwana Daiman Mbeya.
Hata hivyo Katibu kata CHADEMA amesema hawajachelea kuhamia chama hicho kwani ndicho kitakacho wakomboa kifikra na mawazo.
0 comments:
Post a Comment