Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama, akizungumza na watoto waishio katika mazingira hatarishi Airport, Kata ya Iyela Jijini Mbeya, siku ya Ijumaa Kuu April 6 mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama, akizungumza na Mkuu wa Kituo cha mahabusu ya gereza la watoto watukutu lililopo Kabwe Kata ya Iyela Jijini Mbeya, Ijumaa Kuu April 6 mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama, akihutupia watoto katika Kituo cha mahabusu ya gereza la watoto watukutu lililopo Kabwe Kata ya Iyela Jijini Mbeya, Ijumaa Kuu April 6 mwaka huu, ambapo aliwataka kubadilika tabia.
Sehemu ya msaada uliotolewa na Mkuu huyo wa wilaya Bwana Balama katika Kituo cha mahabusu ya gereza la watoto watukutu lililopo Kabwe Kata ya Iyela Jijini Mbeya, Ijumaa Kuu April 6 mwaka huu, kwa jili ya kusheherekea Sikukuu ya Pasaka.
Mkuu wa wilaya Bwana Balama akikabidhi misaada hiyo kwa Mkuu wa Kituo cha mahabusu gereza la watoto watukutu.
******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Watoto watukutu walioko katika Gereza la watoto Kabwe Jijini Mbeya wametakiwa kubadilisha tabia zao za utukutu pindi wanapofikishwa mahala hapo ili waweze kuwa raia wema hivyo kuendelea na maisha ya kawaida kwa ajili ya ujenzi wa Taifa.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Evans Balama alipowatembelea watoto hao kwa lengo la kuwapa moyo na kuwapatia vitu mbalimbali katika kusherehekea sikukuu ya pasaka pamoja.
Balama amesema kuwa Serikali ina nia njema na watoto hao ndio maana inafanya utaratibu wa kuwaweka pamoja ili kuwafundia maadili na utu wema ndani ya jamii ili baadaye wapatikane viongozi bora watakaoweza kuongoza nchi.
Amesema kuwa serikali inajua kuwa miongoni mwa watoto hao wapo madaktari,wanasheria na hata wakuu wa wilaya wa baadaye hivyo wanahitaji kubadili tabia ili wanaporudi katika familia zao wawe raia wema.
Kwa upande wao watoto hao wamemshukuru Mkuu wa wilaya kwa moyo wa kuwatembelea na kusema kuwa hawatamani kuishi katika mazingira hayo lakini wanalazimika kutokana na hali halisi huku wakiahidi kuwa watoto wema na watii pindi watakaporudi uraiani.
Wakati huo huo Bwana Balama ametembelea kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi cha Hallam kilichopo Kata ya Ihyela,Jijini hapa na kuwapa msaada wa chakula katika kusherehekea sikuu ya pasaka.
Akizungumza na viongozi wa kituo hicho Balama amesema kuwa wakati umefika kwa watanzania wenye uwezo kujitoa kwa hali na mali kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu ili waweze kutimiza ndoto zao.
Amesema kuwa jukumu la kulea watoto hawa ni la watazania wote ni si mtu mmoja na kumshukuru Makamu Mwenyekiti wa Hallam Odilia Kyoma kwa kujitoa kwake kwao kuwalea watoto hao pasi kutegemea ufadhili kutoka nje ya nchi bali kwa kuitegemea jamii inayowazunguka.
Aidha,katika maeneo yote mawili vimetolewa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 1.3 kwa watoto hao ikiwa ni ishara ya Mkuu wa Wilaya hiyo kushiriki pamoja sikukuu ya pasaka na watoto hao. Vitu hivyo ni pamoja na mchele,vinywaji aina ya malta,mafuta ya kupikia,sukari,majani ya chai na chimvi.
0 comments:
Post a Comment