Habari na Ezekiel Kamanga,Rungwe.
Bibi mmoja(Ajuza) Mkazi wa Kijiji cha
Kilasi,Kata ya Luteba,Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya Bi.Bestauni
Kagenda(60), amejeruhiwa vibaya baada ya kuvamiwa na bundi wapatao 8
alipoingia nyumbani kwake wakati akitokea kuteka maji mtoni.
Bibi huyo alikubwa na mkasa huo baada
ya kufungua mlango majira ya saa 12:00 jioni Mei 30 mwaka huu na
kukutana na kundi la bundi hao, ambapo walianza kumvamia sehemu
mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu makali.
Aidha Bi Kagenda amesema wakati
akitoka kuelekea kuyateka maji mtoni alikuta bunti hao wameketi eneo la
makazi yake na walipomuona walianza kumshambulia mwilini.
Hata hivyo tukio hilo limearifiwa kwa
Mzee wa Kimila,ambapo waliitisha mkutano wa hadhara na kuonya juu ya
vitendo vya kishirikina na kupinga maovu yote yanayotokea katika jamii
hiyo.
Wakati huohuo Chifu wa Kinyakyusa
Bwana Angasisye Asani amewataka wakazi wa eneo hilo kuachana na mila
potofu, hali inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani kwa wakazi wa
kijiji hicho.
Naye Mwenyekiti wa kijiji Bwana
Asangalwisye Kahole amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba
anawaachia wazee wa mila ili wabaini tatizo linalowakabili.
Mbali na tukio hilo umezuka ugonjwa
wa ajabu wa kuwashwa mwili mzima unaoambatana na upele kwa wanafunzi na
baadhi ya wakazi wa Kijiji hicho cha Kilasi.
Akiongea kwa masikitiko makubwa
Mwenyekiti huyo Bwana Kahole amesema tangu ugonjwa huo uvamie kijijini
hapo ni juma moja sasa ambapo wanafunzi wa shule mbalimbali kijijini
hapo hawaendi shule kutokana na adha ya ugonjwa huo.
0 comments:
Post a Comment