Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Mkazi
wa Kitongoji cha Mayewa,Kijiji cha Masanyila,Kata ya Igamba,Wilaya ya
Mbozi Mkoani Mbeya amegoma mwili wa nduguye marehemu Onesha
Nkota(Shilomanda) mwenye umri kati ya miaka 75 mpaka 80 kuzikwa katika
jeneza.
Sakata
hilo lililotokea Juni 27 mwaka huu majira ya saa nane mchana baada ya
marehemu kufariki na Serikali ya kijiji chini ya Mwenyekiti wake Bwana
Nelson Mgode ulifanya jitihada za kuchonga jeneza lilogharimu shilingi
40,000 na kuliwasilisha nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya maziko.
Lakini
badala ya kushukuru kwa wanakijiji kwa msaada huo,ndugu huyo wa
marehemu alilikataa akidai kuwa kutokana na umri mkubwa marehemu alikula
madawa mengi,hivyo yataidhuru familia yake na kwamba juyo tayari
nduguye kuzikwa kwa jeneza.
Aidha
siku hiyo hiyo,baada ya familia kutafakarei kwa yote yaliyotokea
waliamua kumuomba radhi mwennyekiti wa kijiji lakini alikataa,bali
mwenyekiti alidai uitishwe mkutano wa hadhara aombwe mbele ya wananchi.
Kufutia
hatua hiyo majira ya saa nane mchana mkutano uliitishwa na Bwana Mgode
kuomba radhi na kutakiwa kulipa gharama zilizotumika kutengenezea jeneza
na ng'ombe mmoka kama adhabu ya kuwadharau wanakijiji.
Hata
hivyo Bwana Mgode alilipa gharama hizo na ng'ombe mmoja aliyechinjwa
siku hiyo hiyo na jeneza kukabidhiwa katika uongozi wa machifu kwa ajili
ya taratibu nyingine za kimila huku ndugu zake wakimlaumu kwa
kuendekeza imani za kishirikina.
0 comments:
Post a Comment