Pages


Home » » WACHUNGAJI KUTOKA WILAYA YA MOMBA MKOANI MBEYA WAITAKA SERIKALI KUKUSANYA NYARAKA ZA UCHOCHEZI.

WACHUNGAJI KUTOKA WILAYA YA MOMBA MKOANI MBEYA WAITAKA SERIKALI KUKUSANYA NYARAKA ZA UCHOCHEZI.

Kamanga na Matukio | 04:49 | 0 comments
Mwenyekiti wa kikao hicho Mchungaji Gideon Neema Mwamafupa(kulia) na Katibu wake Padre Isaac Mbanga(kushoto).
Wachungaji wa madhehebu mbalimbali.
*Waipa siku 7 kutekeleza.
*Serikali kubuluzwa mahakamani.

*Wasomali wazagaa Tunduma,Polisi na Idara ya uhamiaji lawamani.

******
Habari kamili na Ezekiel Kamanga,Momba.
Wachungaji wa madhehebu ya kikristo,Wilaya ya Momba,Mkoani Mbeya wameipa siku saba Serikali kukusanya nyaraka za uchochezinchini zinazoendelea kusambazwa na baadhi ya waumini wanaojiita wenye msimamo mkali wa dini ya kiislamu.

Tukio hilo limetokea juzi katika Ukumbi wa Kanisa la Kilutheli  Tanzania(KKKT) Usharika wa Tunduma na kujumuisha wachungaji,wainjilisti,walimu na mapadre wa madhehebu yote ya kikristo yaliyopo wilayani humo.

Mwenyekiti wa kikao hicho Gideon Neema Mwamafupa na Katibu wake Padre Isaac Mbanga,walipokea maoni kutoka kwa wachungaji walioongea kwa uchungu kufuatia Serikali kukaa kimya kutokana na matamko na usambazaji wa CD za uchochezi dhidi ya wakristo nchini na kwamba kitendo hicho wanakiona ni ukiukwaji wa haki za binadamu na kukiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha wachungaji wamesema Serikali imekiuka Ibara ya 50 ya katiba,kifungu cha 15 na 146 sura ya 4 kuhusiana na madaraka ya Umma,ambapo Serikali imeruhusu kujengwa misikiti katika vituo bya mafuta vya oil com nchini hali ambayo ni hatari kwa usalama.

Pia wanesema wamekera na kitendo cha wasomali kuzagaa katika mji huo,huku Maafisa wa polisi na uhamiaji wakiwaangalia tu wakiwa hawana kazina hawana hata Vibali vya kuishi nchini,lakini ifikapo saa saba huenda katika msikiti wa Oil Com na kufanya ibada.

Hata hivyo wamekuwa wakishinda katika baadhi ya nyumba za watanzania waliopo mpakani(Tunduma) na hivyo kutishia usalama wa taifa letu.

Wachungaji hao wamesema kuwa endapo Serikali haitatekeleza maagizo hayo wataipeleka mahakamani kwa sababu imeshindwa kusimamia Katiba na hii imetia wasiwasi hata kule Zanzibar kuchomwa kwa makanisa kunatia hofu usalama wao na kwamba kwa sasa hawapo tayari kunyanyasika tena

Wakati huohuo mpaka sasa wameshakusanya CD na Vijarida vilivyochapishwa kuhusiana na uchochezi,ambavyo vilioneshwa katika kikao hicho.

Mwisho walimaliza kwa kutoa tamko kuanzia Juni 12 hadi 19 mwaka huu,kama hakuna hatua za makusudi kudhibiti hali hiyo wataandamana nchi nzima kudai haki zao.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger