Pages


Home » » AFARIKI DUNIA BAADA YA KUDONDOKEWA NA MBAO KWENYE GARI, WAWILI WAKAMATWA NA BANGI NA 14 WAKAMATWA NA POMBE HARAMU AINA YA GONGO.

AFARIKI DUNIA BAADA YA KUDONDOKEWA NA MBAO KWENYE GARI, WAWILI WAKAMATWA NA BANGI NA 14 WAKAMATWA NA POMBE HARAMU AINA YA GONGO.

Kamanga na Matukio | 01:41 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga,Chunya.
Mkazi wa Kijiji cha Lualanje,Wilaya ya Chunya,Mkoani Mbeya Sani Mgavi(28),ambaye ni mwenyeji wa Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa,amefariki dunia baada ya kudondokewa na mbao wakati akijaribu kuruka kwenye gari.

Tukio hilo la marehemu ambaye ni Fundi wa kupasua mbao,limetokea Juni 7 mwaka huu,majira ya saa 2:30 asubuhi katika kijiji hicho.

Marehemu amefariki wakati alipokuwa akisafirisha mbao hizo na yeye akiwa nyuma ya gari aina ya Fuso lenye nambari za usajili T 732 BWV,mali ya Bwana Joseph Paulo lililokuwa likiendeshwa na dereva Silvesta Simkonda(48) wote ni wakazi wa wilaya hiyo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Diwani Athuman,amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari kukwama kwenye mchanga na kuegamia upande mmoja,hali iliyompelekea marehemu kujaribu kuruka ndipo mbao hizo zilipo mdondokea na kufariki papo hapo.

Hata hivyo mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Chunya na jeshi la polisi linamshikilia dereva wa gari hilo kwa mahojiano zaidi.

Wakati huo huo Jeshi hilo linawashikilia watu wawili kwa kosa la kukutwa na bangi gramu 15, tukio lililotokea Juni 7 mwaka huu majira ya saa 12:55 jioni eneo la Machinjioni,Wilaya ya Rungwe.

Kamanda Diwani amewataja waliokamatwa kuwa ni pamoja na Damas David(31) na Lusekelo Mwakalomba,ambapo hujihusisha na uuzaji na matumizi ya bangi hizo na wote wapo mahabusu.

Aidha majira ya saa 10:45 jioni siku hiyo hiyo maeneo ya Katumba wilayani humo,Polisi walimkamata Bi.Sophia Luvanda(40) pamoja na wenzake 14 wakiwa na pombe ya moshi(Gongo) lita 4 na mtambo mmoja wa kutengeneza pombe hiyo.

Watuhumiwa ni wauzaji na wanywaji wa pombe haramu ya Gongo na mpaka sasa wote wapo mahabusu wakati upelelezi ukiendelea kuhusiana na tukio hilo na mara baada ya upelezi kukamilika watafikishwa mahakamani kusomewa mashitaka yanayowakabili.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger