Pages


Home » » MFUME DUME WAATHIRI HALI YA UCHUMI KWA WANAWAKE.

MFUME DUME WAATHIRI HALI YA UCHUMI KWA WANAWAKE.

Kamanga na Matukio | 05:34 | 0 comments
Habari na Ester Macha,Mbeya.
Kushamiri kwa mfumo dume katika wilaya ya Mbeya kunaathiri kwa kiasi kikubwa hali ya kiuchumi kwa wanawake ambao ndio nguvu kazi kubwa katika kilimo, kipato wanmachopata baada ya mavuno huishia mikononi mwa wanaume wanaojihusiusha na vitendo vya starehe na kusahau malezi ya familia zao.

Uchunguzi uliofanywa na Majira kwa takribani wiki moja  kwa msaada wa mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP)umegundua kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji na ukatili wanavyofanyiwa wanawake wa vijiji vya Ifiga,Iwalanje na Nsongwi juu  Kata ya Ijombe vinavyotokana na nguvu ya wanaume ya kuhodhi mali zilizopatikana kwa kuwashirikisha wanawake.

Mmoja wa awanawake wa Kijiji cha Ifiga Bi Salah Jailos alisema kuwa wakati wa  msimu wa kilimo unapowadia  hushirikiana na waume zao kwa karibu bila kuwepo ugomvi wowote ndani ya familia zao mpaka  mazao yanapokomaa.

Alisema kuwa inapofika kipindi cha kuvuna wanaume  huanza kubadilika kwa kutafuta sababu mbali mbali  za kuonyesha chuki ndani ya nyumba ili aweze kupata sababu za kuvuna peke yake mazao na kuuza pepe yake bila kumshirikisha mke wake.

“Hali hii inatusikitisha sana kwani akishauza mazao haya huondoka nyumbani na kwenda kufanya starehe zake na wanawake wengine, lakini fedha baada ya kuisha hurudi nyumbani na kuanza kutafuta visababu vidogo vidogo kwa kuanza kudai chakula na kutoa sababu mbali mbali ikiwa  ni pamoja  na kudai kuwa chakula kibichi mara hufai kuishi na mimi mara nataka kuoa mke mwingine maadamu tu apate sababu za kujitetea ili mwanamke nionekane mbaya”alisema mwanamke huyo.

Mwanamke mwingine mkazi wa Usongwe Juu Bi.Benadeta Hamisi alisema kufutia vitendo hivyo vya wanaume tunaomba waache kwani iweje wakati wa kilimo  tulime wote lakini inapofika wakati wa mavuno wawe wababe wa kuuza mazao9 peke yao kwa ujumla huu ni ukatili wa kijinsia kwa sisi wanawake wa Kata ya Ijombe.

“Tunaomba waume zetu waache tabia hii kwani mazao haya tunalima sote hivyo hata wakati wa kuvuna inatakiwa tuwe pamoja na hata kuuza vile vile inatakiwa kusimama kwa pamoja kama mke na mume ioli fedha hizo zitakapopatikana mazao  na kuuza yaweze kusaidia kulea familia zetu pamoja na kusomesha”alisema Bi. Hamis.

Hata hivyo mwanamke huyo alisema athari ambazo wanapata baada ya kuachiwa familia ni kupata shida ya  kuhudumia familia ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto namahitaji mengine ya nyumbani ambayo ni muhimu.

Akizungumzia malalamiko hayo kwa Wanawake wa vijiji hivyo, Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Ifiga Bw.Raphael  Siyejele alisema hana taarifa za kiofisi za wanaume kuwanyanyasa wake zao labda kama zipo ngazi zingine.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger