Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mwanafunzi wa Kidato
cha nne,shule ya sekondari Nyerere,iliyopo Mji mdogo wa Tunduma,Wilaya
ya Momba,Mkoani Mbeya Boaz Mwalusanya(18) amefariki dunia baada ya
kujinyonga.
Tukio hilo limetokea
baada ya ugomvi uliokuwepo shuleni hapo,mapema majira ya saa mbili
asubuhi Juni 5 mwaka huu,kabla ya mkutano wa wazazi uliotakiwa uanze
majira ya saa 5 asubuhi siku hiyo hiyo.
Diwani wa Kata ya
Tunduma Mheshimiwa Frank Mwakajoka,amesema marehemu alijinyonga baada ya
kutumiwa kuwa ni miongoni mwa wanafunzi walioanzisha
vurugu,zilizopelekea ugomvi mkubwa uliohusishwa na silaha za visu,hivyo
kusababisha majeraha kwa baadhi ya wanafunzi.
Katika vurugu hizo baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo walitorokea Wilaya ya Nakonde nchi jirani ya Zambia.
Miongoni mwa wanafunzi
waliojeruhiwa na visu ni pamoja na Abel Ndihesya(17) na Asifiwe
Kiungulia(16) wote ni wanafunzi wa kidato cha nne,ambapo walikimbilia
katika Kituo cha Afya cha Tunduma na hali zao zinaendelea vizuri.
Chanzo cha ugomvi baina
ya wanafunzi shuleni hapo hakijaweza kufahamika,ambapo Walimu kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi wanafanya uchunguzi ili kubaini hali
iliyosababisha mchafuko shuleni hapo.
Aidha Jeshi hilo lina
mshikilia mwanafunzi mmoja Mloli(19),anayesoma kidato cha nne katika
shule hizo kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo.
Kwa upande wake diwani
wa kata hiyo mheshimiwa Mwakajoka,amewataka wazazi wa wanafunzi wa shule
hiyo kukutana mapema haraka iwezekanavyo ili kurejesha amani shuleni
hapo.
Miongozi mwa sababu za
magomvi shuleni hapo baina ya wanafunzi ilitokana na baadhi yao kudaiwa
wanatumia vileo na uvutaji wa bangi hali inayosababisha kutokuwepo kwa
usikivu kwa walimu na kuleta vurugu kwa wanafunzi wenzao na pindi
wanapokatazwa kuwatishia.
Mgogoro umedumu shuleni
hapo kwa siku kadhaa na imechangia walimu na wanafunzi kutopatikana na
kudhorotesha mfumo mzima wa uwajibikaji kwao.
0 comments:
Post a Comment