Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abas Kandoro akihimiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake
******
Habari na Angelica Sullusi,Mbeya.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amesema mkoa wa Mbeya ambao ni watatu
kitaifa kwa kuwa na asilimia kubwa ya maambuzi ya virusi vya Ukimwi
(VVU) unahitaji mafunzo zaidi ili kuepusha maambuzi mapya ya ugonjwa
huo.
Kandoro
ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la UKIMWI lililoandaliwa na
Chuo Kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya na kushirikisha wanafunzi zaidi ya
1000 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya Juu vilivyopo mkoani hapa.
Amesema
Mkoa wa Mbeya una maambukizi makubwa ya VVU ambayo yanafikia asilimia
9.2 kiwango ambacho ni kikubwa kulinganisha na wastani wa maambukizi ya
VVU kitaifa ambayo ni 5.7.
Amesema
wakazi wa Mkoa wa Mbeya wanahitaji elimu zaidi ya maambukizi ya VVU ili
kupunguza asilimia hiyo na pia kuwaepusha kupata maambuzi mapya
kutokana na mkoa huo kuwa na majirani ambao wana asilimia kubwa zaidi ya
maambuzi ya ugonjwa huo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Dk Ernest Kihanga amesema kuwa Uongozi
wa Chuo kwa kushirikiana na Serikali ya wanafunzi wameanzisha sera ya
kupambana na ukimwi ili kuwakinga wanafunzi wasipate maambuki mapya ya
VVU wawapo chuoni hapo.
0 comments:
Post a Comment