Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM),alipokuwa ametembelea Chuo Kikuu Cha Teofilo Kisanji(TEKU).
*******
Habari na Angelica Sullusi,Mbeya.
Chama
cha Mapinduzi (CCM) kimesema bado kinaendelea na mchakato wa kuwaondoa
madarakani wanachama wake wenye tuhuma za ufisadi na wale wasiokuwa na
maadili mazuri kwa jamii, maarufu kwa jina la kuvua gamba.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye Jijini Mbeya alipozungumza na
waandishi wa habari Jijini hapa.
Nape
amesema kuwa dhana ya kujivua gamba ilipangwa kuwa na awamu tatu,
ambapo awamu ya kwanza ya kuwataka wahusika wawajibike wenyewe na
imepita ingawa ilikuwa na mwitikio mdogo.
Kwa
mujibu wa Nape awamu ya pili ya kujivua gamba ilipangwa kufanyika
kupitia uchaguzi wa ndani ya chama hicho, na kuwa awamu hiyo ndio sasa
inaendelea.
Amesema
awamu ya tatu ni ya kuwawajibisha wahusika kupitia vikao vya chama,
ambapo mpaka sasa tayari vikao vya kuwajadili viongozi wa juu wa chama
hicho wenye tuhuma za ufisadi vimeanza na vitakapokamilika umma
utashuhudia mageuzi makubwa ya uongozi wa chama hicho kikongwe nchini.
Aidha,
Nape amesema katika awamu ya pili ya kujivua gamba ambayo inahusisha
wanachama wote kutoa maamuzi kupitia uchaguzi, mchujo mkali utapitishwa
kwa watakaoomba kugomea nafasi mbalimbali za uongozi, ambapo wale wenye
tuhuma majina yao hayatarudi.
0 comments:
Post a Comment