Na. Shomi Mtaki, Tunduma
Tabia ya viongozi wa Chadema kuchanganya masualaya yaushabiki wa
kisiasa na kufitinisha wananchi na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) katika mikutano yake vya hadhara pamoja na vikao vya baraza la
halmashauri ya mji wa Tunduma wlayani Momba, nusura kiongozi mmoja wa
chama apate kipigo.
Kiongozi
huyoi Frank Mwakajoka ambaye ni diwani wa kata ya Tunduma (Chadema),
alinusulika kipigo hichojana kutoka kwa wajumbe wa Baraza la
Halmashauri ya Mji huo baada ya kuwatukana wajumbe katika kikao hicho
kilichafanyikia ndani ya ukumbi wa hoteli ya Flamingo mjini hapa.
Tukio
hilo lilitokea katika kikao hicho kufuatia hoja ya mwenyekiti wa mtaa
wa Tukuyu Kenneth Mwankuga, kutaka ufafanuzi wa kauli za viongozi wa
Chadema, kudai katika mkutano wa hadhara uliofanyika hivikaribuni katika
mtaa wake kuwazushia uongo viongozi wa CCM kuwa wameuza soko la
Majengo.
Mwankugha
alisema viongozi hao akiwemo diwani huyo walifanya mkutano wa hadhara,
katika eneo hilo na kuenezauzushi huo na kudai kuwa uongozi wa Chadema
umepinga hatua hiyo jambo ambalo halikuwa sahihi.
Hivyo
kupitia Baraza hili naomba nipate ufafanuzi ili zaidi ili niwapelekee
wananchi majibu sahihi maana viongozi hao tunao katika kikao hiki,”
alisema Mwankuga.
Hoa
hiyo iliungwa mkono na wajumbe wengine wanaotokana na CCM na kumtaja
diwani huyo kuwa ndiye aliyetamka maneno hayo na kuwa amekuwa na tabia
ya kutengeneza uchochezi kila mara anapofanya mikutano ya hadhara mjni
hapa.
Wajumbe
hao walisema diwani huyo akishirikiana na viongozi wa chama chake,
amekuwa mstari wa mbele kusababisha kutoweka kwa amani na kuzusha vurugu
zisizo za msingi zinazojitokeza mara kwa mara katika mji huo
Hata
hivyo maneno hayo yalimfanya diwani huyo asimame na kuanza kukanusha
taarifa hiyo kwa madai kuwa yeye ndiye aliyekuwa akitetea kufuatia
kuwepo kwa taarifa hizo.
Hata
hivyuo diweani huyo alianza kutoa lugha chafu dhidi ya wajumbe wa
mkutano huo akisema,“acheni ujinga wenu,hakuna mnachosali mtaendelea
kubaki hivyo hivyo na tena nawaambieni kesho (leo) nitaitisha mkutano
mwingine niwaambie wananchi ujinga wenu” alisema.
Wakati
diwani huyo akiendelea kuongea, kelele za wajumbe hao na baadhi ya wa
Chadema walianza mzozo huku wajumbe wengine wakiwa wamemzonga diwani
huyo kwa lengo la kumpa kipigo kufuatia kauli zake hizo,ambazo
hazikuwaridhisha baadhi ya wajumbe wa baraza hilo.
Mzozo
huo uliochukua takribani dakika 20, ulifanya hali ya kikao kutoeleweka
ambapo baadhi ya wajumbe walitaharuki na kuwaondolea utulivu kufuatia
kuendelea kulizungumzia jambo hilo badala ya kujadili agenda zilizo
mbele yao.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan
Mwanshiga alikanusha kuwapo kwa jambo hilo na kuwataka wajumbe
wasiingize mambo ya mtaani kwenye vikao badala yake wawe makini kujadili
mambo ya msingi.
Akizungumzia suala hilo Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),ta ya Tunduma Hemed Steven aliwataka wajumbe hao kuacha kuingiza Siasa kwenye vikao vya maendeleo badala yake wafanye majukumu waliyotumwa na wananchi.
“Tujue
siasa inatumika wapi na wapi ni masuala ya maendeleo haya yaliyotokea
mimi nasema wajumbe watambue majukumu waliyotumwa na wananchi huo ndiyo
ujumbe wangu sina zaidi I have no comment ”alisema Steven.
Naye
Mwenyekiti wa Jimbo la Magharibi Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Joseph Mwachembe alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema CCM watambue kuwa
chadema hakiwezi kuwasifia bali kitaendelea kuwafitinisha na wananchi.
0 comments:
Post a Comment