Habari na Ezekiel Kamanga,Tunduma.
Wakazi
wa mtaa wa Mwaka Kati,Kata ya Tunduma,Wilaya ya Momba,Mkoani Mbeya
wameifunga Ofisi ya Mwenyekiti ya mtaa,kutonana na wananchi hao kuikataa
taarifa ya mapato na matumizi.
Tukio
hilo limetokea Juni 11 mwaka huu,majira ya saa tano asubuhi,wananchi
hao waliamua kuweka kufuli jingine na kufanya ofisi hiyo kuwa na
makufuli mawili,hali iliyopelekea mwenyekiti huyo kushindwa kuingia
ofisini kwake.
Sakata
hilo limekuja kufuatia mkutano wa hadhara uliofanyika mwishoni mwa
mwezi Mei mwaka huu,uliokuwa na lengo la kusoma mapato na matumizi ya
mataa kwa wananchi ambapo taarifa hiyo waliikataa iliyosomwa na
Mwenyekiti wa mtaa huo Bwna Elias Cheyo na kumtaka ajiuzuru lakini
alilikataa agizo hilo na kuondoka mkutanoni.
Kufuatia
dhahama hiyo Mwenyekiti huyo aliamua kufungua mashtaka mahakamani na
wananchi watatu wanashikiliwa kwa kosa la kutishia kuua kwa maneno,na
kusomesha shtaka katika mahakama ya mwanzo Tunduma.
Aidha
watu hao wamelikana kosa hilo hali ambayo ilipelekea kesi kuahirishwa
mpaka Juni 11 mwaka ambapo mlalamikaji Bwana Cheyo,hakufika mahakamani
hapo baada ya kutoa udhuru kwamba anaumwa.
Kesi hiyo imesogezwa mbele mpaka Julai 19 mwaka huu ndipo itakaposikilizwa tena katika mahakama hiyo.
Hata
hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi kadhaa walionekana
katika Mji huo wakiwa na mabango mbalimbali ya kulaani kitendo cha
kutosomwa taarifa ya mapato na matumizi,hususani uvunjwaji wa kamati ya
maendeleo ya ujenzi wa shule na ufujwaji wa pesa za makusanyo ya
michango kutoka kwa wazazi.
0 comments:
Post a Comment