Habari na Angelica Sullusi,Mbeya.
Baadhi ya wananchi mkoani Mbeya wametaka bajeti ya
Serikali inayotarajiwa kusomwa Bungeni wiki ijayo isaidie kupunguza mfumuko wa
bei nchini ili kuwapunguzia wananchi makali ya maisha.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hii kwa nyakati
tofauti Jijini Mbeya, wanachi hao wamesema kuwa mfumko wa bei ndio chanzo
kikubwa cha watanzania kuwa na maisha magumu, hivyo Serikali inapaswa kulipatia
tatizo hilo
kipaumbele katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha.
Waziri Elimu wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu
cha Teofilo Kisanji,Bwana Milanzi Petro amesema ili bajeti ijayo iwanufaishe
wananchi, ni lazima wizara zinazoigusa jamii moja kwa moja zipewe kipaumbele
ili ziwe na uwezo wa kuwahudumia wananchi.
Amesema ili kupunguza tatizo la mfumko wa bei Serikali
itoe kipaumbele cha bajeti kwenye wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ili iwe
na uwezo wa kuwahudumia wananchi katika kuinua kilimo na hatimaye kuongeza
uzalishaji wa mazao na kupunguza bei za mazao.
Nae, Mwanafunzi wa mwaka wa mwisho katika Chuo Kikuu
Huria (OUT) Tawi la Mbeya,Bwana Eddo Mwamalala amesema kuwa bejeti ijayo
inapaswa kuja na vitu vitakavyosaidia kupunguza na kudhibiti mfumuko wa bei.
Wiki ijayo vikao vya Bunge la 10 la Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania
vinaanza mjini Dodoma
kwa ajili ya kupokea, kujadili na kupitisha makadirio ya bajeti ya Serikali kwa
mwaka wa fedha wa 2012/13.
0 comments:
Post a Comment