*Afisa mtendaji wa Kata akaa kwenye kituo zaidi ya miaka 20.
*Afisa Mtendaji wa Kijiji naye ajimegea shilingi 380,000.
Mkataba
wa ahadi ya kulipa fedha kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha
Masanyila,anaedaiwa kufuja pesa taslimu shilingi 2,350,000 za zahanati
ya kijiji.
******
Habari kamili na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
******
Habari kamili na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Masanyila,Kata ya Igamba,Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya
Bwana Chepson Mkanjilwa,anatuhumiwa kuiba pesa taslimu 2,350,000,kati ya
shilingi milioni 12 zilizotolewa na Halmshauri ya Mbozi kwa ajili ya
ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho iliyogharimu zaisi ya miliozi 24
lakini mpaka sasa haija kamilika.
Katika
katika mkutano uliofanyiaka Julai 21 mwaka 2011 mwenyekiti
huyo,alikirikutumia pesa hizo kwa matumizi yake binafsi na alipobanwa
siku hiyo alitoa shilingi laki mbili na salio la 2,150,000 kuahidi mbele
ya mkutano huo wa hadhara kwa uthibitisho wa kuweka saini kwenye barua
ya mkataba mbele ya Afisa mtendaji wa kijiji hicho Bwana Justin Mgala
lakini hajazirejesha.
Kufuatia
hatua hiyo Wenyeviti wa vitongoji 6 vya Kijiji hicho walikutana na
kumwalika Diwani wa Kata hiyo mheshimiwa Amos Kalonge,lakini hali
ilikuwa ndivyo sivyo kutokana na mwenyekiti na afisa mtendaji wa kijiji
kuingia mitini.
Katika
hali hiyo isiyokuwa ya kawaida Afisa mtendaji Bwana Mgala,anatuhumiwa
kwa kufuja shilingi 380,000 alizokabidhiwa na Mkandarasi kwa ajili ya
kununulia mchanga wa kujengea nyumba ya Daktari wa zahanati ya kijiji na
mpaka sasa haonekani ofisini kwake,licha ya kupewa uhamisho kwenda
kijiji kingine huku wananchi wakiwa hawajui la kufanya.
Kwa
upande wake Mheshimiwa Kalonge,aliwataka viongozi hao na wananchi
kuahirisha mkutano huo hadi Juni 27 mwaka huu na atamuomba Mkurugenzi wa
Halmashauri na Mkuu wa Wilaya ili waweze kusikiliza kero za wananchi wa
kijiji hicho.
Aidha,wananchi
hao wamemtupia lawama Afisa Mtendaji wa kata hiyo Bwana Ambakisye
Waya,,ambaye amedumu katika kata hiyo kwa takribani miaka 20 sasa na
kudai kuwa amekifanya kijiji kama mradi wake wa kufuja fedha kupitia
watendaji wa vijiji na akishatimiza azma yake huwahamisha watendaji hao
vituo vya kazi hali inayopelekeza pesa za wananchi kupotea ovyo.
Hata
hivyo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Bwana
Levson Chilewa,amekiri kupokea malalamiko ya kijiji hicho na kwamba
ofisi yake ilituma mkaguzi hivyo taarifa yake ataitoa siku za hivi
karibuni.
0 comments:
Post a Comment