Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk. Norman Sigalla akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kufukuzwa kazi kwa madaktari hao. |
Mkurugenzi wa wa hospitali ya rufaa Mbeya Dr E. Sankey akimsikiliza kwa makini kaimu mkuu wa mkoa Mbeya
*******
|
Habari na Godfrey Kahango,Mbeya.
Sakata
la mgomo wa Madaktari katika hospitali ya Rufaa Mbeya, limeendelea
kuingia katika sura mpya baada ya Madaktari 72, waliogoma kutimuliwa na
bodi ya hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya.
Hatua
ya kutimuliwa kwa madaktari hao imekuja baada ya bodi hiyo kuwaandikia
barua ya kuwataka kukaa meza moja na kujadili mstakabali mzima wa
madai yao ambapo wadaktari hao kukaidi wito huo.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
ambaye pia ni mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dr. Norman Sigalla, alisema kuwa
wameamua kusitisha Mkataba wa madaktari hao na kuwarudisha kwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kuchukuliwa hatua za
kinidhamu.
”Madaktari
54 ni wale walioko kwenye mafunzo ya vitendo kwa mkataba wa miaka
miwili na hospitali ya Rufaa na madaktari 18 ni wale walioajiriwa na
Wizara ya afya” alisema Sigalla na kuwataka wale wote wanaoishi bwenini
hospitalini hapo kuwa ifakapo saa 11:00 jioni ya leo(jana) wawe
wameondoka katika eneo hilo la hospitali”alisema.
Alisema
kuwa wamefikia hatua hiyo kwa kuwa madaktari hao wamekiuka , kuvunja
mkataba wawalioingia na hospitali hiyo pia kukiuka kanuni za kudumu za
Umma na toleo la 2009, kifungu namba F16- F. 17 na F27.
Alisema
kuwa madaktari hao waliandikiwa barua ya mara ya kwanza ya kuwaita ili
wakutane na Mwenyekiti wa bodi hiyo ya rufaa mbeya lakini walikaidi na
kuandikiwa barua ya pili ya kuwataka waeleze kwa nini wasichukuliwe
hatua za kinidhamu kwa kutofika kazini kwa siku tano lakini nayo
waliikaidi.
Dr.
Sigalla akizungumzia kuhusu madaktari 18 ambao ni waajiriwa pia wamo
katika mgomo huo alisema kuwa nao wanakabidhiwa barua zao za
kusimamishwa ajira zao hospitalini hapo na kuwarudisha Wizarani kwa
katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kwa hatua stahiki za
kinidhamu.
“Madaktari
waajiriwa wanakabidhiwa barua zao za kusimamishwa ajira yao hospitalini
hapa na kuwarudisha Wizarani kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii kwa hatua stahiki za kinidhamu” alisema Dr. Sigalla.
Hata
hivyo gazeti hili lilishuhudia baadhi ya madaktari hao wakiondoka
kwenye mabweni yao huku madaktari hao wakisikika wakisema wapo tayari
kurudi walikotoka na kwamba hawapo kuvumilia kile kinachoendelea hivi
sasa.
“Tupo
tayari kuondoka hospitalini hapa na kurudi tuliko toka wala hatutishiki
hata kidogo” walisikika wakisema huku wakiwa wanapakia mabegi yao
kwenye tax walizokodi.
Wakati huohuo Jeshi la Polisi mkoania hapa lilizingira eneo la Hospitali ya Rufaa kuimarisha ulinzi na usalama.
0 comments:
Post a Comment