Mshindi nambari moja Winfrida Paulo(katikati) akifuatiwa na mshindi wa pili Sabrina Abdul(kulia) na Mshindi nambari tatu Careen Elias(Kushoto),katika
Mashindano ya Miss Redds Mbeya 2012,ambapo Warembo 12 kutoka wilaya
zote za mkoa wa Mbeya walishindani taji hilo. Tukio lililoandaliwa na
Kituo cha Redio Bomba FM 104.0Mhz Mbeya na kudhaminiwa na Kampuni ya TBL kupitia kinywaji
chake cha Redds, SBC Tanzania LTD kupitia kinywaji cha Mountain Dew,
Masasi Fashion, Access Computer LTD, Beaco Resort, Grace College, Shaba
Pub na Mfikemo Hotel na litasindikizwa na burudani toka kundi la Coast
Modern Taarab a.k.a Watafiti wa mipasho.
Mshindi wa Taji la Miss Redds Mbeya
2012 Winfrida Paulo aliyekati muda mfupi baada ya kuvishwa taji hilo na
aliyekuwa Miss Mbeya 2011(bluu), katika Ukumbi wa Mkapa uliopo Jijini
Mbeya na kusindikizwa na Burudani kutoka Kundi nzima la Mambo ya Mwambao
Coast Modern Taarab kutoka Jijini Dar es Salaam.
Pichani aliyekuwa Miss Mbeya
2011(gauni la bluu), akimvisha taji alilotwaa mwaka jana Mshindi wa Miss
Redds Mbeya 2012 Winfrida Paulo.
Washindi wa nafasi ya 1,2 na 3 wa
Miss Mbeya 2011 wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya
kukabidhi mataji hayo kwa washindi wa Miss Redds Mbeya 2012.
Warembo walioingia katika Tano bora ya washiriki wa shindano la Miss Redds Mbeya 2012, ambpo jumla ya warembo 12 kutoka wilaya za
jiji warembo 5, Mbeya vijijini warembo 3 , Mbalali 1, Chunya 1 na Mbozi
mshiriki 1 walipanda katika jukwaa moja.
Wasanii wa Kundi la Coast Modern
Taarab a.k.a Watafiti wa Mipasho akiwemo Kibibi Yahaya(Kulia),Mauwa
Tego(wa pili kutoka kulia), wakitoa burudani katika shindano la Miss
Redds Mbeya 2012, lililoudhuriwa na wakazi wengi wa Mkoa wa Mbeya.
Wasanii na wapiga vyombo wa Kundi la Coast Modern Taarab a.k.a Watafiti wa Mipasho
akiwemo Omary Tego(aliyevalia suti rangi bya maziwa) wakiwa katika picha ya pamoja kablya ya kutoa
burudani katika shindano la Miss Redds Mbeya 2012, lililoudhuriwa na
wakazi wengi wa Mkoa wa Mbeya.
Mgeni rasmi katika Shindano la Miss
Redds Mbeya 2012 Bwana Geofrey Anania,ambaye pia ni Katibu tawala wa
Wilaya ya Mbeya akizungumza wakati wa shindano hilo.
Sehemu ya mashabiki waliohudhuria shindano hilo.
Sehemu ya mashabiki waliohudhuria shindano hilo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Adili(kulia),ambaye pia ni Mkurugenzi wa Chapakazi Production iliyopo jijini Mbeya.
*****Usikose kutembelea kesho kupata mwendelezo wa matukio mbalimbali ya shindano hili***** Hisani ya Chimbuko Letu Blog!!
0 comments:
Post a Comment