Na mwandishi wetu.
Mwenyekiti
wa haki za binadamu mkoa wa Mbeya Said Mohammed amesema watoto wa kike
waishio wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya,wamekuwa wakikosa haki ya msingi ya
kielimu kutokana na wazazi kuwaozesha watoto wao wakiwa wadogo.
Ameyasema
hayo wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hii,ofisini kwake na
kuongeza kuwa ndoa za utotoni zimekuwa chanzo kikubwa kwa watoto
kushindwa kuendelea na masomo.
Aidha
amesema pamoja na Serikali kuwa na mkakati wa kuwawezesha watoto wa
kike kielimu jitihada hizo zimekuwa zikishindikana kutokana na ndoa za
utotoni na wazazi kuwaficha watu wanaohusika kuwapatia ujauzito watoto
wao.
Kuhusu
hatua za kisheria zinazochukuliwa na Serikali Bwana Mohammed amesema
inakuwa ni vigumu kuzitambua kutokana na mchakato wa kesi hiyo kuwa
mgumu kwa sababu ya wazazi kushindwa kutoa ushahidi mahakamani.
0 comments:
Post a Comment