Baadhi
ya majeraha yaliyotokana na kipigo kwenye mwili wa marehemu Daniel
Godluck Mwakyusa (31) ambaye alikuwa mwanachuo wa Chuo Kikuu cha Teofilo
Kisanji(TEKU),Mbeya aliyeuawa na Askari wa Jeshi la Polisi mkoani hapa
tarehe 14/02/2012 katika sikukuu ya wapendanao {valentine day].
******
Habari na Mwandishi wetu.
Kesi ya mwanafunzi anayedaiwa kuuawa na Polisi Mkoani Mbeya,itaanza kusikika Juni 27 mwaka huu katika Mahakama Kuu,jijini Mbeya.
Mwanachuo
huyo anayedaiwa kuuawa na Polisi marehemu Daniel Mwakyusa,aliyekuwa
anasoma katika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) kilichopo jijini
hapa,tukio lililotokea Februari 14 mwaka huu.
Imedaiwa
marehemu na wenzake walikuwa katika sherehe ya Siku ya wapendanao
duniani,ambapo marehemu aliuawa mita kadhaa kadhaa kutoka eneo la
Grocery,huku ndugu wakisema marehemu aliuawa kwa sime na risasi kama
inavyodaiwa na Jeshi la Polisi.
Kesi
hiyo ambayo wananchi wengi walikuwa wakifuatilia inahusisha Jeshi la
Polisi mkoani Mbeya kwa kutumia Askari wake ambao ndio wanaodaiwa
kusababisha kifo hicho.
Asasi
mbalimbali zimekuwa zikilalamikia Polisi kujichukulia sheria mmkononi
na kufanya vitendo vya unyanyasaji kwa wananchi wasiokuwa na hatia
badala ya kufuata majukumu yao ya kazi kwa kushirikiana na jamii.
Kwa
upande wake Mzazi wa marehemu,Bwana Godluck Mwakyusa amesema mwanae
alimtegemea sana na tukio hilo limemfanya mara kadhaa kukosa
amani,kufuatia majeraha ambayo mwanae alisababishiwa na Askari waliokuwa
doria siku hiyo.
0 comments:
Post a Comment