Miili ya Marehemu ikiwa tayari imewasili katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.
*******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Maiti 10 kati ya 13 zimetambuliwa na
ndugu,kufuatia ajali iliyotokea juzi Juni 5 mwaka huu Mkoani Mbeya
ikihusisha gari la abiria aina ya Coaster lenye nambari T 886 na gari ya
mizigo aina Lori lenye kichwa nambari T 658 ASJ na tela nambari T 150
BDZ.
Mkuu wa usalama wa barabarani Bi. Butusyo Mwambelo, amewataja marehemu hayo kuwa ni Emmanuel Mwanjala
mkazi wa Ilomba na Uyole jiji la Mbeya,Mwanike Focus mkazi wa Chunya na
Uyole jijini hapa,Lucia Lingson(51) mkazi wa Katumba Wilaya ya Rungwe na
Lena Ngomano(49) mkazi wa Ngumbulu Isongole Wilaya ya Rungwe.
Wengine ni pamoja na Pius Mbeya mkazi
wa Uyole,Mwase Pius makazi wa Iganzo jijini hapa,Bahati Japhari(33)
mkazi wa Kyela,Ernesta Kikanga(62) mkazi wa Ifunda Iringa, Dereva wa
Coaster Mwasa Daimon(40) na Yerusalem Mwakyusa(35) wote ni wakazi wa
Mbeya.
Bi. Mwambelo amesema kuwa maiti
tatu bado hazijaweza kutambuliwa na amewataka ndugu,jamaa na marafiki
ambao ndugu zao hawajaonekana kufika katika Hospitali ya Rufaa kwa
utambuzi wa maiti hizo.
Hata hivyo ameongeza kuwa dereva wa lori aliyesababisha ajali bado hajapatikana na juhudi za kumtafuta bado zinaendelea.
0 comments:
Post a Comment